Kwa mtindo huu hata kama mimi ningekuwa mwalimu nisingefundisha kwa bidii

Nkobe

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2013
Posts
2,204
Reaction score
3,277
Kama ningekuwa mwalimu nikatambua kuwa mbunge anaingiza si chini ya milioni 8 kwa mwezi, anamiliki v8 ndani ya miezi mitatu baada ya uchaguzi, anapewa sitting allowance ya laki mbili, anapewa perdiem mamilioni ya kwenda malaysia kuangalia kilimo cha mpunga wakati mbunge si afisa kilimo (afundishi wakulima), baada ya miaka mitano akistaafu anapwa milioni 50 mimi nimetumikia miaka 30 napewa milioni 13. Nisingekubali kufundisha kwa bidii

Mimi mwalimu nalipwa laki 3 wakati maisha ya hapa mjini kodi ya nyumba laki na nusu kwa mwezi, chakula bei juu, mavazi bei juu, shule bora kwa mwanangu ada milioni 1 kwa mwaka, kwa hali hii nisingefundisha kwa bidii

Wakati niko darasani nafundisha naingiwa na kumbukumbu kuwa niliomba kuongezewa mshahara lakini Serikali ikanipeleka mahakamani. Wakati huohuo nasikia kuwa walioninyima nyongeza ya mshahara wamepeleka mabilioni ya pesa uswis, kwenye mikataba ya gesi Mtwara tayari wamevuna mabilioni ya pesa na kuyakimbizia nje ya nchi. haaa, nisingefundisha kwa bidii

Naingiwa kumbukumbu kuwa kwenye change ya rada wanafunzi wangu wangeletewa vitabu angalau wanafunzi wangu wafanye home work zao vizuri, lakini mpaka sasa sisikii tena hizo pesa zimekwenda wapi. Hii ingenipunguzia kasi ya kufundisha

Nikiwa naandaa leson plan, nasikia mbunge wangu aliepewa uwaziri amejenga nyumba ya dola 400,000 (sawa na milioni 600) na hakuna hatua imechukuliwa kweli nakata tamaa ya kufundisha.

Nikiwa napata ugumu jinsi ya kubajet mshahara wangu wa laki 3, mara nasikia kiongozi wangu mabilioni ya fedha anayaita vijisent.Hii nayo inanikatisha tamaa ya kufundisha kwa bidii
 

Usilaumu Wabunge tu; laumu mfumo mzima, kuanzia: Mkuu wa Idara, DEO, REO, Wizara ya Elimu, nk.
 

Haya ni mawazo ya mtu aliyekata tamaa. kama ingekuwa hivyo hata Rais wa tanzania asingekubali kuwa rais kwa watu walalamishi na wasiyopenda kufanyakazi kiasi hiki. Fanyakazi kazi mkuu, peleka watoto shule wasije wakakata tamaa kama wewe.
 
Bunge dhaifu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na seikali iliyo chini ya CCM ndio chanzo kikuu cha ukichaa na kuchanganyikiwa kwa sekta ya elimu ya nchi hii.
"Walimu tuna hali ngumu, japo tuna umuhimu".
 

Ndiyo maana haujawa mwalimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…