Kwa mujibu wa Lissu, kumbe hata Majaji hawalipi kodi!

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,828
Reaction score
165,667
Katika akaunti ya twitter ya Mhe. John Heche,kuna clip ya Lissu ambapo Lissu anaonekana alikuwa anaongelea suala la mishahara ya wafanyakazi ambapo amesema Majaji wote wa nchi hii hawalipi/hawakatwi kodi kwa mujibu wa sheria.

Katika clip hiyo, Lissu anaonekana kusikitishwa na makato makubwa yanayowakabili watumishi wa umma na kupinga Majaji kutokatwa kodi kutoka katika mishahara yao.

Maoni yangu:
Ingawa clip hiyo inaonekana ni ya siku za nyuma na imekuwa retweeted tu leo hii na Mhe. Heche, huu kwangu ni ushahidi tosha wa Lissu kuja kubadili hali hii iwapo atapitishwa na kuwa mgombea uraisi kupitia CHADEMA na kisha akaja kumshinda Magufuli(kwa uwezo wa Mungu inawezekana hata kama Tume si huru).

Vile vile naamini itakuwa ni mwanzo wa Raisi wa nchi hii nae kukatwa kodi katika mshahara wake.

Mwaka huu watanzania msifanye makosa.

 
Unapoteza muda wako bure. Lissu hawezi kuwa Rais wa JMT labda rais wa Chadema. Kama anaweza aende porini akawe rais huko!!
 
Unapoteza muda wako bure. Lissu hawezi kuwa Rais wa JMT labda rais wa Chadema. Kama anaweza aende porini akawe rais huko!!
Kama unaihakika na hilo, kubalini tume huru ya uchaguzi. Utaona kitakachompata huyo mwenyekiti wako anaejiita kichaa
 
Lissu atakuwa kiongozi bora sana.... nchi ili iendelee inahitaji kutawaliwa kwa mujibu wa sheria...

Huwezi Kunitukana hadharani kisa tu eti wewe boss wangu...
Aisee labda walinzi wako waniwahi ila kwangu lazima ule gumi moja kali
la bichwa ili iwe fundisho na mimi nikafie jela.

Utawala wa sheria ni kiungo muhimu sana kati ya watawala na watawaliwa.
 
Mabeberu wamemkataa huyo muongo muongo na Magu ashamprove wrong mara nyingi sana.
Mnatumia nguvu nyingi kumpa promo ninyi makada wa CHADEMA ili tumjadili humu; HATUTAKI!
 
Kwani wabunge hawalipi kodi?
 
Unapoteza muda wako bure. Lissu hawezi kuwa Rais wa JMT labda rais wa Chadema. Kama anaweza aende porini akawe rais huko!!
Hata Magu hakuna aliekuwa anawaza kuwa angekuewa Rais baada ya Kikwete.

Hata leo hakuna aliekuwa anawaza kwamba Mkapa anaweza kuwa marehemu.

Hata Lissu wengi hawakutarajia angepona ila ndio hivyo.

Isitoshe,hakumtarajia na mpaka sasa hamuamini kuwa Lissu anarudi.

Binadamu na kiumbe dhaifu, kwahiyo funga domo lako usije kuumbuka siku moja kwani hujui kesho nini kinaweza tokeo.
 
Unapoteza muda wako bure. Lissu hawezi kuwa Rais wa JMT labda rais wa Chadema. Kama anaweza aende porini akawe rais huko!!
Sawa.... Lakini wote tukatwe kodi

Ova
 
Narudia tena kwa msisitizo Lissu hawezi kuwa Rais wa nchi hii full stop labda baada ya miaka 50.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…