Wakuu leo katika pitapita za hapa na pale mtandaoni nimekutana na hii kauli ya Naibu Katibu Mkuu CHADEMA-Bara, Benson Kigaila kuwa idadi ya watanzania ni milioni 64 kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.
Benson Kigaila, Naibu Katibu Mkuu CHADEMA-BaraJe uhalisia wa hili ni upi wakuu?
Benson Kigaila, Naibu Katibu Mkuu CHADEMA-Bara
- Tunachokijua
- Benson Kigaila ni naibu katibu mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) taifa ambaye amekuwa ni moja kati ya viongozi ambao wamekua watetezi wa masuala ya kidemokrasia na haki za binadamu nchini. Kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa novemba 2024. Kigaila amekuwa akisema na kukemea bila kuogopa ukiukwaji wa taratibu za kidemokrasia ambapo kumekuwepo kasoro zinazolalamikiwa kuelekea uchaguzi huo.
Mnamo tarehe 04 Novemba 2024, Benson Kigaila pamoja na Godbless Lema, mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya kaskazini walifanya mkutano na waandishi wa habari wakizungumzia mwenendo wa mchakato kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa 2024, ambapo mambo yaliyozungumzwa ni zoezi la uandikishaji pamoja na uchukuaji na urejeshaji wa fomu kwa wagombea.
Akizungumzia takwimu za uandikishaji zoezi lililofanyika kuanzia Oktoba 11, mpaka Oktoba 20, 2024 Kigaila alisema watanzania tupo milioni 64 kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.
Ni upi uhalisia wa idadi hiyo ya watanzania?
Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa si kweli kwamba Tanzania ina jumla ya watu milioni 64 kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.
Kwa mujibu wa tovuti ya tume ya taifa ya takwimu (NBS) ambapo inaonesha takwimu juu ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 Tanzania ina jumla ya watu milioni sitini na moja laki saba na elfu arobaini na moja mia moja ishirini (61,741,120) wanaume wakiwa 30,053,130 na wanawake 31,687,990.
Hivyo kauli ya Kigaila kuwa Tanzania ina watu milioni 64 akirejelea sensa ya 2022 sio kweli kwani tofauti na takwimu halisi.