Mhimili uliojichimbia
Senior Member
- Jul 2, 2017
- 172
- 191
Bila ya kupoteza muda niende moja kwa moja kwenye lengo la uzi huu. Wiki iliyopita nilimsikiliza mkurugenzi wa ufundi wa shirikisho la soka Tanzania (TFF) mtaalamu wa kimataifa wa kuinua na kuvinoa vipaji ndugu Ammy Ninje akihojia katika kipindi cha nyundo ya Baruani Azam tv, pamoja na mambo mengi aliyozungumza sehemu kubwa ikihusisha historia yake ila ningependa kujadili jambo moja ambalo limeniuma kama mdau wa michezo hasa kabumbu.
Ndugu Ninje alizungumzia suala la timu yetu ya Serengeti boys (U-17) ikiwa sisi ni wenyeji wa mashindano ya AFCON-U17 yanayotarajiwa kufanyika mwezi April 2019 hapa Tanzania, kinachoshangaza ni kuwa hadi leo timu haipo kambini sio hilo tu pia haijulikani lini itaingia kambini na wala hakuna wadhamini/mdhamini na shirikisho halijapokea fedha ya kuendeshea timu hiyo na lipo na hali mbaya kiasi kwamba hata yeye hiyo kazi anayofanya kwa sasa anajitolea tena kaacha kazi yenye mshahara mnono Uingereza kuja kuinua soka la bongo.
Hivi kwa mwendo huu tunatarajia soka letu litafika wapi? Tunaenda kushindana na giants kutoka west africa sijui nini kitatokea.
Hapa ndipo utagundua kuwa matatizo yaliyopo kwenye ligi zetu hasa premier na pia timu ya taifa na vilabu vyetu kutofanya vizur kimataifa yana mzizi mrefu.
Kama kwenye hili ambalo sisi sio washiriki tu bali pia ni waandaaji wa mashindano tupo na mwendo huu ambao hata kobe katuzidi mbio, lakini tunatarajia kwenda World cup-u17, ambapo tiketi ya kwenda huko inatokana na kufanya vizuri hapo april hivi tupo serious na suala la michezo(soka) kweli au tunataka tuwe wasindikizaji kila mwaka?
Sent using Jamii Forums mobile app