Kwa mwendo huu soka letu litaishia maneno tu

Mhimili uliojichimbia

Senior Member
Joined
Jul 2, 2017
Posts
172
Reaction score
191
Bila ya kupoteza muda niende moja kwa moja kwenye lengo la uzi huu. Wiki iliyopita nilimsikiliza mkurugenzi wa ufundi wa shirikisho la soka Tanzania (TFF) mtaalamu wa kimataifa wa kuinua na kuvinoa vipaji ndugu Ammy Ninje akihojia katika kipindi cha nyundo ya Baruani Azam tv, pamoja na mambo mengi aliyozungumza sehemu kubwa ikihusisha historia yake ila ningependa kujadili jambo moja ambalo limeniuma kama mdau wa michezo hasa kabumbu.

Ndugu Ninje alizungumzia suala la timu yetu ya Serengeti boys (U-17) ikiwa sisi ni wenyeji wa mashindano ya AFCON-U17 yanayotarajiwa kufanyika mwezi April 2019 hapa Tanzania, kinachoshangaza ni kuwa hadi leo timu haipo kambini sio hilo tu pia haijulikani lini itaingia kambini na wala hakuna wadhamini/mdhamini na shirikisho halijapokea fedha ya kuendeshea timu hiyo na lipo na hali mbaya kiasi kwamba hata yeye hiyo kazi anayofanya kwa sasa anajitolea tena kaacha kazi yenye mshahara mnono Uingereza kuja kuinua soka la bongo.

Hivi kwa mwendo huu tunatarajia soka letu litafika wapi? Tunaenda kushindana na giants kutoka west africa sijui nini kitatokea.

Hapa ndipo utagundua kuwa matatizo yaliyopo kwenye ligi zetu hasa premier na pia timu ya taifa na vilabu vyetu kutofanya vizur kimataifa yana mzizi mrefu.

Kama kwenye hili ambalo sisi sio washiriki tu bali pia ni waandaaji wa mashindano tupo na mwendo huu ambao hata kobe katuzidi mbio, lakini tunatarajia kwenda World cup-u17, ambapo tiketi ya kwenda huko inatokana na kufanya vizuri hapo april hivi tupo serious na suala la michezo(soka) kweli au tunataka tuwe wasindikizaji kila mwaka?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Timu ya taifa kwa namna moja ama nyingine lazima ipewe sapoti na serikali sasa viongozi sa iv wamejificha wanasubiri timu ifike nusu fainal au finali ndyo wajitokeze na ahadi kedekede

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu hii TFF ya akina Karia haina sifa ya ku intertain wadhamin...zero personalities, vision, strategies, innovation etc


Sent from my itel it1556 Plus using JamiiForums mobile app
 
Rais wa TFF ni mwanasiasa sio mtu wa mpira badala ya kutafuta Wafadhili anahangaika kumkatia Rufaa Wambura

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shekhe timu iko kambini katika hostel za TFF pale karume,Mimi nilienda juzi nikawakuta vijana pale .

Labda hukumsikiliza vizuri huyo bwana,au pengine alikuwa anasema hivyo ili apate wadhamini ,lakini timu iko kambini.

Pia,wakati wa malinzi nakumbuka kuna pesa za FIFA zilitoka kwa ajili ya timu ya taifa ya wanawake,malinzi akasema sehemu ya pesa hizo pia zitapelekwa timu. ya vijana.
 
Mkuu hayo mahojiano yapo U tube nilisikiliza several times wala sijasikia vibaya, may be timu ilikusanywa faster baada ya kuona aibu ya kilichozungumzwa, kwani jamaa alisema anatumaini hao watoto waliko wawe wanajiandaa individually ili wasipoteze fitness.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…