Tetesi: Kwa mwenye ufahamu na hili.

Tetesi: Kwa mwenye ufahamu na hili.

R Mbuna

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2015
Posts
2,283
Reaction score
5,371
Habari za Leo wakuu.

Kuna habari nimezisikia kuhusu gharama za kujifungua kwa wamama wajawazito. Hapo awali mama mjazito anapofikia wakati wa kujifungua anatakiwa awe na vifaa tu vya kujifungulia iwapo ataenda hospital za serikali na hatochangia hata senti.

Ila jana kuna mtu amenipa habari kuwa kwa sasa hivi watakaoenda kujifungua kwenye hospitali za serikali wanatakiwa kuchangia kiasi cha pesa.

Kwa wale watakaozaa bila upasuaji watalipia kiasi cha shilingi 80,000/ ( Elfu themanini) na wale watakaohitajika upasuaji itawagharimu kuchangi takribani laki mbili.

Nilikuwa naomba kujua uhakika wa maelezo haya isiwe watu wanaposha kwa maana bado tupo kwenye mapambano ya kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi hasa wakati wa kujifungua.

Iliwekwa kujifungua bure ili kuhamasisha wanawake wasijifungulie nyumbani ukizingatia uchumi pia ulikuwa changamoto.

Nawasilisha .
 
Hata kama ni milioni tafuta sehemu nzuri mke ajifungulie. Ww ulimshona mimba utegemee azae bure
 
Mkuu mke wangu si mjamzito by the way huwa sipendi sana vya bure halafu sijiangalii Mimi tu.

Huwa naangalia sana watu wa vijijini ambao serikali ilikuwa inawahamasisha waache kuzalishana majumbani ili kupunguza idadi ya vifo vya mama na mtoto.

So nilihitaji kujua ukweli wa hizi tetesi kama haujui nawe tulia wenye kujua waje kutujuza.
Hata kama ni milioni tafuta sehemu nzuri mke ajifungulie. Ww ulimshona mimba utegemee azae bure
 
Wakati wa kampeni tuliambiwa watajifungua bure na watoto chini ya miaka mitano watatibiwa bure
 
Back
Top Bottom