Kwa mwenye ufahamu wa mishahara ya wapiga picha (wachanganya picha) kwenye hizi media binafsi

Kwa mwenye ufahamu wa mishahara ya wapiga picha (wachanganya picha) kwenye hizi media binafsi

Mingendeu

Senior Member
Joined
Aug 26, 2019
Posts
115
Reaction score
237
Kuna kijana amehitimu maswala ya videography na target yake ni kwenda kwenye hizi media Kama wasafi, clouds, eatv etc . (Anachangamoto/ majukumu kidogo kweny familia ijapokuwa hana kipato cha kueleweka)

Kutokana na maisha yalivyo ni muhimu kufahamu hata mishahara tu ya waliopo kweny ajira inasomaje ili nae ajipime Kama itaweza kumkwamua au afikirie namna nyingine ya kufanya.

Kwa mwenye ufahamu wa mishahara ya wapiga picha (wachanganya picha) kwenye hizi media binafsi anaweza kuwa Msada Sana. Level ya elimu ni shahada ya kwanza.

Natanguliza shukrani .
 
Kabla ya kuuliza mshahara, unaworking experience ya over 5 five years?
Kama huna hili swali lako ni batili
 
Kabla ya kuuliza mshahara, unaworking experience ya over 5 five years?
Kama huna hili swali lako ni batili
Hana. Lakini unaweza kusaidia kwa kujibu hata mwenye hiyo experience ya miaka 5 anaweza kulipwaje, na less ya 5yrs anaweza kulipwaje ili apate mliganyo.

Private sector ni kawaida Sana hata kufanya kazi miaka 5 bila nyongeza yoyote, hivyo ni vyema kuangalia kianzia chako cha awali bila kuweka matarajio makubwa kwenye nyongeza. (Kama uliwahi kupita kampuni za kihind unaweza kunielewa kidogo)
 
Ushauri wangu ni bora akaingia kwenye utalii, ila sasa hapo atafute kwanza camera yake binafsi ya maana na nyingi zinaanzia walau milioni 4.

Ila kwenye utalii akijituma atapata kampuni za kufanya nazo kazi na uhakika wa kufika mbali zaidi.

Akumbuke pesa inaletwa na vitu vifuatavyo, juhudi, maarifa na pesa yenyewe.

Kila la heri.
 
Kikubwa awe a sehm ya kula awa jamaa mishaara awalip mpka miez 3 na point
Hivi huwa na mikataba rasmi au ndio Kama vibarua tu?? Hii ya kutolipwa kwa muda fulani huwa naisikiaga sana lakini sijawahi kuelewa inakuaje mtu mwenye mkataba asilipwe miez kadhaa na anaendelea na kazi tu?? Anawezaje kujikimu? Kwann hashitaki??
 
Hiyo hipo mkuu wanakuambia tutakulipa sasa utafanyeje?
 
Back
Top Bottom