Natumai mko salama,
Dhumuni la Uzi huu ni kuwaomba wadau wote wenye Uzoefu na Usafirishaji wa Bidhaa mbali mbali kwenda Kuuza Nje ya Nchi, Haswa Bidhaa za Vyakula na Matunda.
Ningependa Kujua ni Hatua gani zinachukuliwa Kuanzia hapa Nchini mpaka Huko Nchi Husika
Kwa Mfano mimi Nahitaji Kujua namna ya Ku Export Zao la Zabibu Nyeupe na Vanilla
Kuna mdau aliwahi kuandika hapa Jf kuwa kuna Wakenya huwa wanaenda Dodoma kununua hizo Zabibu kisha wanazi Re Pack na Kuzisafirisha kwenda Spain, kwa mwenye taarifa zaid basi atuwekee hapa
Mtanisamehe kwa Mpangilio wa Uandishi na Natanguliza Shukrani
Mwamba.