Kwa namna hii kuna haja ya kuwa na marafiki kweli?

Ni kweli kuna marafiki sio marafiki bali ni maadui na hawapaswi kabisa kuaminiwa.
Unaweza kumkopesha na akaahidi kukulipa ndani ya muda fulani na badala yake muda unapita. Mbaya zaidi hata simu hapokei!

Sasa, ukiamua kumpa hela ndg, jamaa au rafiki, ni afadhali ujiandae kisaikolojia ikiwa atakurudishia au asipokurudishia.
Haya mambo ya kukosa uaminifu yanaathiri sana kisaikolojia. Baadhi wanafikia hadi kuchanganyikiwa sababu ya kudhulumiwa! Usikubali hili likuathiri kisaikolojia; badala yake pambania malengo yako! Litapita tu!
 
Usikopeshe marafiki kama huna nguvu ya kudai.
 
Mkuu biashara ya miamala ya kifedha si ya siri, anaona unavyobadilishana pesa na wateja, kwa hiyo kwenye mazingira ya dharura sana na kwa kudhani kuwa wataona umuhimu wa kutokuangusha biashara unavaa ubinadamu na kutoa pesa, lakini kumbe wao fikra zao zipo tofauti kabisa na tatizo linaanzia hapo
 
Very sure...tatizo ni watu nipo nao ofisini kila siku yaani
 
Pole sana mkuu, mara nyingi binadamu huwa tunajifunza kutokana na maumivu.

Mimi nakushauri usisitishe urafiki, at least sio kwa style hiyo. Wazungu wana msemo wao kwamba, "Do what you must, your friends will adjust."

Mimi ilinikuta situation kama hiyo, nilichokifanya, kwasababu ya hasira na maumivu, nikaanza kuwa muwazi - namfuata mtu uso kwa uso, namwambia bila kupepesa macho kwamba alichokifanya sio sawa na sijakipenda, na kumwambia natumaini atarekebisha mara moja. Mara nyingi reaction huwa ni yule mtu kukujengea chuki, lakini taratibu somo linamuingia, na mwisho yeye mwenyewe aidha atajiondoa katika orodha ya marafiki zako, au kama ni muungwana atakuja kuomba radhi, atarekebisha alichokosea na hatarudia tena kukopa kwako, na atakuwa balozi kwa wengine.

Ukiwa mkweli na muwazi kiasi hicho, hulazimiki kudanganya kuwa huna hela au biashara mbaya n.k., kwasababu wanajua mzee hupepesi macho, wala hupindishi maneno pale mtu akikuzingua. Hali hiyo inawafanya waogope kuja kuazima pesa kizembe. Na mtu akiazima basi atakosa uhuru kiasi ambacho ataona bora ahamishe deni, akope kwa mwingine alipe kwako ili aishi kwa amani... maana akikuona tu anaanza kujieleza kabla hata hujamuuliza.

Pia, mimi binafsi huwa sioni shida kumwambia mtu, "Mara nyingi nikimuazima mtu pesa huwa harudishi. Unaonaje tukiweka collateral ambayo itafidia kama usiporudisha kwa wakati ulioahidi" Na wananijua, namaanisha ninachosema na ninasema ninachomaanisha.

Ukiwa na tabia hii, mwanzoni watakusema sana, lakini baada ya muda wataelewa kuwa wewe ni mtu mwenye misimamo yako hasa linapokuja suala la pesa. Kwahiyo kama ni urafiki watajiondoa wenyewe kwa kujua kuwa hawatawezana na wewe kwa style hiyo. Mwisho utajikuta umebaki na rafiki mmoja au wawili ambao wao ni marafiki zako katika yote... uwe huna wapo, ukiwa nacho wapo, uwape pesa wapo... uwanyime wapo.

Mimi... ninashukuru.
 
Mimi bwana nlishajifunza sitaki kabisa kupendwa sana na kila mtu.

Jamani nawaambieni tena. Watu hawalipi madeni.....nishapitia machungu mengi sijui niwaambie nn muelewe....acha kukopesha watu hela kaza uonekane una roho mbaya its fine....ila mjue watu hawalipi madeni jamani...

Kuna kiasi kama 2M nilipoteza kwa usxxge kama huu yani. F@ken Sanaa.

Kuna li sxxge flani mpaka nikaapa kabisa hata lije kupatwa na msiba sitakaa nilipe tena pesa yangu......kwanza ni mtu anapenda makuu sanaa kuishi maisha ya gharama kuonekana ana maisha mazuri alaf hela hana na kupenda kuhemea mifuko ya wengine....nikaja mchana ukweli maisha unayoishi blo kama hujaja kuf!r_@ mjini hapa sijui nakuambia.

Tufanyeni kazi jamani...maisha yanahitaji nidhamu sanaa.
 
Kwani hela ni zako ama za biashara?bora ufuate hiyo njia unayotaka kuifuata usiwe karibu na ndugu na marafiki, kwa sababu biashara yako itakufa na wameshajua wewe ni rafiki yao mjinga mjinga (dumbest)
 
Km anakuzonga zonga na hutaki kelele zake za maudhi Mkopeshe tu!! ili umdai vizuri na ili asije kwako tena kukubanabana kuna marafiki wengine ving'ang'anizi sana!
 
Ahsante sana mkuu, this is the real meaning of our presence, nimeuchukua ushauri wako...
 
Kwani hela ni zako ama za biashara?bora ufuate hiyo njia unayotaka kuifuata usiwe karibu na ndugu na marafiki, kwa sababu biashara yako itakufa na wameshajua wewe ni rafiki yao mjinga mjinga (dumbest)
Duuuh...kusaidia mtu wakati wa matatizo kumbe pia ni ujinga ujinga?
 
Nakubaliana na wewe kabisa, ila marafiki wanapokuja wakiwa na shida nzito na wanajua kabisa uwezo wa kuwasaidia kusolve matatizo kwa dharura, ila kwanini hawawezi kufikiria kwa utu tu na kurudisha kwa uaminifuuuu????
Ndio maana wanasemaga kua bora umfadhili mbuzi kwan mwanadam anayomaudhi...... . wengi wetu huwa hatukumbuki fadhila, endapo mtu akiona amekidhi shida yake hakumbuki alipo saidika.... ndio maana njia fupi tu ya kuepuka yote hayo ni linapokuja swala la pesa katika msaada wewe msaidie kwa kiwango chako na si kukopesha. Sahau neno KUKOPESHA kwenye pesa sahau!!
 
Km anakuzonga zonga na hutaki kelele zake za maudhi Mkopeshe tu!! ili umdai vizuri na ili asije kwako tena kukubanabana kuna marafiki wengine ving'ang'anizi sana!
ni kweli ving'ang'anizi wapo ila kama hupendi mabishano na ugomvi we mpe tena kiasi tu kidogo kwa kumsaidia na si kumkopesha zaidi ya hapo labda kama upo tayari kwa shari kipindi atakapoanza chenga.
 
Hii kanuni hua naitumia sana,nakopesha ambacho ntakuwa tayari kupoteza
 
Nakuelewa sana Mkuu,Dawa nyingne ni kumuambia akitaka 400,000 Mwambie hio pesa sina na kwa kujibana kwa ajili yako utaweza kumpa labda 100,000.
Mpe sababu kua ulipatwa na matatizo au unamarejesho
 
Nakuelewa sana Mkuu,Dawa nyingne ni kumuambia akitaka 400,000 Mwambie hio pesa sina na kwa kujibana kwa ajili yako utaweza kumpa labda 100,000.
Mpe sababu kua ulipatwa na matatizo au unamarejesho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…