Kwa namna ilivyo ni bora katiba itafasiriwe kwa umakini ili kulinda maslahi ya umma

Kwa namna ilivyo ni bora katiba itafasiriwe kwa umakini ili kulinda maslahi ya umma

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
6,404
Reaction score
6,969
Kwa mujibu wa ibara ya 67(1)(b) mbunge awe na sifa kamili za kuwa mbunge ni lazima aidhiniswhe na chama chake kugombea ubunge.

Mdee na wenzake 18 ni dhahiri na wazi kabisa hawana sifa hiyo.

Ibara ya 107A ya katiba ya JMT inatamka wazi kabisa kuwa mahakama ndio chombo pekee kilicho na mamlaka ya kutoa haki hapa nchini.

Halima na wenzake walikosa uhalali wa kuwa wabunge mara tu baada ya kufutwa uanachama wa Chadema.

Suala la wao kugombea uhalali wa kufutwa uanachama wao lilipaswa kuendelea mahakamani huku wao wakiwa wamefutwa uanachama. Maana tukio la kwanza kabisa ni kufutwa uanachama wao.

Kwa namna yoyote ile hakuna budi kukipa kipaumbele kifungu cha 107A na 107B kwa manufaa ya taifa letu.

Chadema ni matapeli wa kisiasa.
 
Kwa mujibu wa ibara ya 67(1)(b) mbunge awe na sifa kamili za kuwa mbunge ni lazima aidhiniswhe na chama chake kugombea ubunge.

Mdee na wenzake 18 ni dhahiri na wazi kabisa hawana sifa hiyo...
Muulize spika wako ana order from court inayozuia Mh.Mdee&others wasiachishwe ubunge?,elewa mahakama ni kimbilio la kudai haki lakini sio kusikiliza au kuhukumu kesi za kisiasa, na elewa vyama vya siasa ni vya hiari!huwezi lazimisha kuwemo
 
Back
Top Bottom