Kwa nilichokiona na kukisikia leo nathibitisha rasmi kuwa Tanzania hatuna 'Critical Journalists' bali tuna 'PR and Round Table Journalists' tu

Hii ni awamu ya tano katika kipindi chake cha pili cha miaka Kumi !!. Awamu ya sita itaanza baada ya awamu hii ya tano kufikia ukomo wake... October 2025. Vingenevyo swali lako lingemtoa kwenye reli.
 
Hal
Tusiwalaumu huenda walipewa script ya kuuliza maswali,ole wako uulize nje ya script[emoji23]
Halafu upo uwanja wa ugenini๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ wamuulize msigwa kule iringa mbele ya hayati alijiona hatoshi๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Nafikiri bado kuna kitu hakipo sawa, wanatesti mitambo, kuna uvumi unasema msitu ni mpya komba ni wale wale.....
 
Huyo Balile anajulikana ni mlamba mata.ko maarufu, hakuna anachosimamia zaidi ya maslahi yake binafsi.
 
You are very brave & wise.
Mungu akubariki sana.
 
Mimi ningeuliza hivi:
1. Mheshimiwa, sehemu kubwa ya taarifa za vyombo vya habari ni malalamiko ya vijana kuhusu ukosefu wa ajira. Je, utaratibu ukoje wa Serikali wa kutoa ajira, ni wa moja kwa moja au ni wa kupitia mahojiano? (Interview)
Kama ni wa moja kwa moja, ufanisi wa waajiriwa katika sehemu wanazopangiwa mnautambuaje?
 
1.Awamu iliyopita tulishuhudia kila mwezi ikitoa takwimu za makusanyo kupitia TRA ambapo ni kigezo mojawapo cha uwazi ktk utendaji wa serikali.Nini kinakwamisha utolewaji wa takwimu hizo awamu hii?

2. Siku unapokea report ya CAG na TAKUKURU mwezi march uliagiza uchunguzi wa haraka ufanyike fedha zote zilizotolewa hazina kuanzia January hadi march,lakjni mpaka Leo mwezi wa tatu tangu umeagiza tunaona kimya.

3.Report ya CAG ilibainisha shirika la ndege la ATCL limekua likijiendesha kwa hasara,wakati huo huku bado waziri mkuu akitwambia bado kuna ndege kadhaa zitakuja ili kukamilisha idadi flani hauoni kama kutakua ni kuendeleza hasara?

4.Kwa miaka kadhaa serikali iliyopita wewe ukiwa makamu wake mmekua mkituaminisha kwamba tutembee kifua mbele tuko kwenye right track kiasi ambapo hata kipindi cha wimbi la kwanza la ugonjwa wa uviko tulihakikishiwa kwamba tuna dola reserve za kutosha kuendesha nchi kwa zaidi ya miezi 6 bila kuzalisha,nini kinakwamisha ajira mpya za kutosha ili kuongeza mzunguko wa fedha mtaani(multiplying effect).?

5.Siku ya kongamano UDOM ulikaririwa ukisema wewe na magufuli ni kitu kimoja,MAGUFULI alisema yeye kwake katiba mpya sio kipaumbele na wala katika kampeni zake hakuna alipoinadi,ni UPI msimamo wako juu ya takwa la katiba mpya.

6. Serikali iliyopita wewe ukiwa kama makamu tuliambiwa gas ni yetu lakini kutokana na masharti ya mkataba sisi tunapewa asilimia kidogo ambazo pia zimeshindwa kumaliza tatizo la uhaba wa umeme nchini,lakini juzi ukiwa kenya umekaririwa ukisema tuatanza kuwauzia gas Kenya,INA maana gas ya kuuza ipo lakini ya kuzalisha umeme wa kutosha na kulisha viwanda vyetu hatimae viweze kushindana kibiashara Africa ndo haitoshi.

7.Awamu iliyopita wewe ukiwa makamu tumeshuhudia uvunjwaji mkubwa wa haki za binadamu hadi kuibuka kwa msemo wa wawatu wasiojulikana,umejipangaje kuhakikisha hao waliokua hawajulikani wanajulikana na sheria inachukuliwa dhidi yao.

8.........naendelea kuload maswali mengine Bahat mbaya kadri navofikia hitimisho naona ndivo maswali konk yanazd kuload kichwani.
 
Angalia hata vyombo vya habari vyenyewe vilivyo dhofu mbaya! Hao walijitahidi kuuliza maswali yenye afadhali si unaona na vyombo vyao! "Vyombo vinaamua ubora wa watenda kazi.
Sionagi hata haja ya viongozi kutoa mawsali kwa wanahabari wanaowahoji.
Miongozo na sheria sahihi huzaa uchumi imara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ