Kwa nilivyoteswa na Deo wa Bagamoyo nalaani Mwanangu asisomee kazi ya ualimu

BUMIJA

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2011
Posts
5,950
Reaction score
11,295
Niliripoti na kuanza kazi 2008, na nilianza katika shule ya sek Matipwili huko hifadhi ya saadani.

Ilipofika mwaka 2011 ilikua zamu yangu kwenda kusoma na nikahamishwa shule mpya na wakati nilishaomba chuo na mwezi wa8 Deo akanitamkia airisha mwaka na kwangu kufa na Diploma ilikua ngumu.

Nikaenda ila mshahara ukakatwa na mwaka huu nimemaliza Degree ya Elimu na nimerudi kituoni ndio sasa naanza moja kufatilia mshahara.

Hapa nilipo sina hela naishi kwa mateso kanakwamba najuta hata kua nilisomea ualimu ili nini. Nakula ugali na maharage ya wanafunzi na inabidi mana nimefulia vibnaya mno.

Najua wapo wenye moyo wa kunisaidia hata pesa kidogo nisiteseke. Kwa wenye moyo namba yangu ya mpesa ni 0759063942.

Mashallah
 
Huyo Deo ni nani? Ama unamaanisha D.E.O?
 
Taja jina la afisa elimu ashugulikiwe mapema urudishwe kwenye mshahara yote maana anakuja toka hazina afisa elimu wanagawana na watu wao hazina kuu wanajua wewwe uko kazini na mshahara unapata
 
Mwaka 2011 alikua Majoya na mwaka jana kahamishiwa Wilaya ya Mkuranga na Wa Mkuranga kaletwa Bagamoyo.
 
Barua ya ruhusa ilifika nao wamechelewa kujibu na mie ilikua haifai kuahirisha masomo na sikupata barua ya onyo au kufukuzwa na pia nlifika TSD Wilaya mwaka jana wakadai hawajui lolote.
 
Sio siri halmashauri ya Bagamoyo ni watemi kupita maelezo
 
Huyu admin anasoma bachelor of medical lab pale muhas, sema anataka tu kuuchafua ualimu, sio inshu hivyo wanajf
 
Hii ni thread ya pili au ya tatu kuhusu hili suala lako.Pole ila kwa mchango sahau
 
napata shida kuamini kama una diploma au degree kwani Maandiko yako hayashabiani
 
Mi ni Mwalimu bana na Meningitis mchango wako ni muhimu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…