Mkuu swali hili watu huwa wanalipa majibu mepesi kama yaliyotangulia hapo juu, lakini ambacho wenzetu wamefanya na ambacho sisi hatufanyi ni kwamba wenzetu wamewekeza kwenye technology. Bila teknology hatuwezi kufika huko. Wameanzisha research and develpment institution ambazo ziko integrated na manufacturing. Taasisi za namna hii zinawawezesha kukifanyai vitendo kile ambacho wamekisoma na kukibuni na kinazalishwa kwenda kwa mtumiaji wa mwisho.
Sisi hatujiwekei malengo kama wenzetu, hawa Asian countries wanasoma kwa malengo fulani lakini sisi tunasoma bila malengo ndo maana unakuta madoctor na maprof. wanaongeza vipatao vyao kwa kuanzisha bar, kufuga kuku, kujenga guest house n.k
Inatakiwa tujiwekee malengo kwa mfano kwamba kufikia mwaka fulani nchi ijitosheleze kuzalisha trekta ndogo kwa ajili ya wakulima wetu, tuzalishe vigae vyetu wenyewe, tuunde gari letu wenyewe n.k. Kwa kufanya hivyo tutaandaa wataalamu wa kuwezesha kufikia malengo hayo. Bila malengo makubwa kama hayo hatuwezi kufika popote.
Kwa hiyo ndugu yangu hakuna mmujiza, Asia walifanya hivyo wakajikuta wanazalisha ziada ya kuuza nje ya nchi wakaongeza foreign reserve zao, watu wao wakapata ajira na maisha yao yakaboreka.
Sisi tumeuza viwanda vyote, tukajitoa kwenye public investment na World bank wakatuletea structural adjustment program ambayo ndo inazidi kutufanya masikini zaidi.
To conclude research and development integrated with manufacturing is the answer, what we need and what is mostly lacking in Africa is a visionary leadership to know what i am talking about.[/QU
mkuu umeiba jibu langu,so sina cha kuongeza