samahani mkuu niliandika nikiwa na natumia kasimu kangu ka kuangalia update za humu. sasa naomba leo nieleze kwa ufasaha kwa nini hizi rate za benki zinatofautiana na za bureau de change;..
Niende moja kwa moja kwenye point;
tofauti za kwenye exchange rate kati ya benki na bureau de change ni kutokana na sababu kadhaa;
1. kuleta usawa katika kubadilisha fedha.(to maintain equilibrium) **neno kubadililisha fedha inamanisha kubadili kutoka fedha ya kigeni kuwa ya nyumbani Tanzania au kutoka fedha ya nyumbani Tanzania kuwa ya kigeni**.Tukumbuke kama kusipokuwa na usawa katika kubadilisha fedha itasababisha watu kuwa na uwezo wa kununua fedha sehemu moja na kuuza sehemu nyingine. yaani kununua benki na kuuza kwa bureau de change au kununua kwa bureau de change na kuuza benk. sasa unaona kwenye hizo rate zote hakuna sehemu mtu anaweza kununua na kuuza sehemu nyingine. kwa mfano kama akienda kununua bureau de change atauziwa kama ifuatavyo:
Sanya Bureau de change buy ni 2,225 na sell 2,235
Chelsea Bureau de change buy ni 2,228 na sell 2,240
Jobex Bureau de change buy ni 2,228 na sell 2,240
kuna moja siikumbuki jina ila buy 2,227 na sell 2,238
***maandishi mekundu ni bei ya kununulia pesa ikiwa mtu atauziwa na Bureau de change***
Na akitaka kuuza kwa benki atauza kama ifuatavyo:
CRDB buy ni 2,170.00 na sell 2,280.00
NMB buy ni 2,156.00 na sell 2,276.00
NBC buy ni 2,182.18 na sell 2,292.18
***maandishi mekundu ni bei amabyo muuzaji atatumia kuwauzia benki***
Kama akinunua benki na kuuzia Bureau de change itakuwa vs versa rate ya kununua benk ni sell na rate ya kuuzia Bureau de change ni buy.
kama ukiangalia hizo bei vizuri utagundua kama mtu akinunua benki na kuuza Bureau de change atapata hasara mfano atanunua benk kwa shilingi 2,280 na atauza Bureau de change kwa shilingi 2,225 atapata hasara ya shilingi 55. na akinunua Bureau de change atanunua kwa shilingi 2,235 na atauza benk kwa shilingi 2170 apo atapata hasara ya shilingi 65.
Hapa tukumbuke Bureau de change ni moja ya msambazaji wa fedha kwa rejareja na benki ni msambazaji wa jumla na rejareja. benki anamuuzia Bureau de change fedha kwa jumla na Bureau de change anawauzia wateja wa rejereja mtaani. (natumia neno kununua kuuza kwa sababu vyovyote atakavyofanya kununua au kuuza atafanya kwa faida). ilik kuondoa uwezekanano wa mtu kujiingiza katikati na kupata faida ya kununua upande mmoja na kuuza upande mwingine bei zao zina pishana kama mtoa post alivyoona katika pitapita zake.
Kutaokana na maelezo hayo hapo ni wazi kutofautina huko kutaleta usawa katika kubadilisha fedha kwa kuondoa uwezekano wa mtu kununua sehemu a na kuuza sehemu b kwa lugha ya kitaalam arbitrage opportunity (kiswahihi chake sikifahamu vizuri) .
..........sababu ya pili
itaendelea...