Kwa nini biashara nyingi hushindwa kubaki sokoni katika miaka mitano ya awali toka kuanzishwa?

Joined
Jun 28, 2017
Posts
72
Reaction score
124
Habari wana bodi!
Leo naomba tuangalie miongoni mwa sababu za kwa nini biashara nyingi kushindwa kubaki sokoni kwa ndani ya miaka mitano japo biashara nyingi huenda hata hii miaka mitano ikawa mingi sana toka kuanzishwa kwake na njia ambazo tutaweza kulinda biashara/mitaji isianguke/kufa
Hakuna mjasiriamali anaependa kuanzisha biashara halafu baada ya muda iwe yenye kufa kwani ukiachana na kupoteza 'mtaji' lakini vile vile muda mwingi aliotumia utakuwa wenye kupotea bure na rasilimali mbalimbali alizowekeza nazo zitakuwa zenye kupotea hivyo kupata hasara!
Sababu zipo nyingi lakini kwa kuanza naziona sababu 6 na njia za kutatua matatizo hayo:

1[emoji830]Usimamizi mbovu (poor management skills)
Inatokana na kukosa ujuzi na maarifa ya namna bora ya kuisimamia biashara husika. Msimamizi anashindwa kukabiliana na changamoto katika maeneo ya uzoefu, uamuzi, usimamizi, maono ya biashara unataka ielekee wapi nk. Usimamizi ulio imara ni nguzo muhimu sana katika kukabiliana na changamoto za kuiendesha biashara
■=>Njia ya kutatua hili
Pata ushauri wa kitaalam, kuwa na mtafsiri wa mawazo yako na kuyaboresha 'mentor', usikurupuke kuanzisha biashara kwa sababu ya kusikia inalipa au fulani unamjua anaimudu vema au kuwa na pesa si sababu ya kufanya maamuzi ya biashara kama huna tafiti za kutosha juu ya biashara husika

2[emoji830]Kukosa upekee na thamani
Unaweza kuwa na bidhaa au huduma yenye uhitaji mkubwa sana kwa wateja lakini ukashindwa kusimama katika soko na hatimae biashara ikafa. Hii inatokana na namna ulivyoiingiza bidhaa/huduma katika soko. Namna mbaya ulivyoitambulisha bidhaa/huduma yako katika soko japo ilikuwa na uhitaji mkubwa unaigeuza inakosa thamani na upekee hivyo kushindwa na washindani wako
■=> Njia ya kutatua hili
Jiwekee viwango na vigezo vya kuitambulisha bidhaa/huduma yako katika soko kujitofautisha na washindani wako. Jiulize haya maswali
●je unafanana na washindani wako katika soko?
● je nini cha ziada ambacho una ofa wateja wako?
●je una upekee gani katika huduma/bidhaa yako ambayo wateja hupata?
Hii ndiyo njia ya kutengeneza "BRAND" (chapa) ya bidhaa/huduma utoayo kwa wateja wako. Brand ni mguso au picha ya kipekee ambayo mteja wataitambua na kuitofautisha na bidhaa/huduma nyingine. Chapa inaweza kuwa katika logo, hisia, muundo, mtazamo nk ambayo hawezi mteja akapata katika bidhaa/huduma kutoka kwa washindani wako. Tambukisha bidhaa kwa kufuata njia sahihi na mipango sahihi na hatua sahihi ili ijijenge katika akili za wateja

3[emoji830]Kukosa mvuto kwa mahitaji halisi ya wateja
Biashara itashindwa sokoni kama bidhaa/huduma zako zitakuwa hazina mguso na mvuto wa moja kwa moja kwa mteja. Bidhaa au huduma yako inaweza kupendwa na wateja kwa kuboresha na kubadilisha muonekano na taratibu za upatikanaji wake. Jifunze kuwasikiliza wateja wanasemaje juu ya bidhaa/huduma yako! Je wanatakaje juu ya bidhaa/huduma yako!

■=> Njia y kutatua hili
Jenga utamaduni wa kuwasikiliza wateja na kufanyia kazi yale yasemwayo juu ya bidhaa/huduma utoayo kwao. Angalia wateja wanataka nini? Jenga mfumo imara wa uhusiano kati yako na mteja ie customer relationship management crm kuzuia kuanguka kwa biashara yako. Usilewe sifa bali zidisha maboresho kila unapopata nafasi

4[emoji830]Biashara isiyo na Faida
Kunza biashara kwa mihemko au kusikia au kuiga pasina kufanya upembuzi yakinifu hakika mwisho wake huwa sio mzuri. Hii inatokana na kutokuijua biashara vema nje na ndani, changamoto zake nk. Usifanye biashara pasina kujua kama ina faida kiasi gani na ukikosea inakukata mtaji kwa namna gani. Mfano mdogo unaleta matunda labda maembe mjini ilhali soko limefura bidhaa hiyo mwisho wa siku mzigo unakuharibikia kabla hata ya mauzo kwani hukufanya upembuzi yakinifu wa kujua soko la bidhaa husika nk

■=> Njia y kutatua hili
Pata maelezo ya kutosha juu y biashara unayoifikiria utaiweza, shirikisha wataalam, andika maelezo ya kila habari unayoipata juu ya biashara husika na vlvl andaa mchanganuo wa biashara n mpngokazi kama dira na mwongozo wako

5[emoji830]Matumizi mabovu ya pesa
Kuchanganya matumizi mbali mbali na kushindwa kujitenga kutokna na biashara hivyo kujikuta watumia hela ovyo ni miongoni mwa sababu za biashara nyingi kufa. Ujuzi wa namna bora ya kuandaa mahesabu huwa ni miongoni mwa sababu vile vile. Kutokuwa na kumbukumbu sahihi za mapato na matumizi nk

■=> Njia ya kukabiliana na hili
Jifunze kuweka rekodi mbali mbali za mauzo, mapato na gharama zozote unazoingia ili mwisho ujue nini unapata. Tumia wataalam wa mahesabu katika kupata njia bora na nzuri zaidi za kutumia pesa. Jitenge na biashara kwa kujiwekea mipaka katika matumizi ya pesa ikiwa pamoja na kujilipa mshahara sahihi

6[emoji830]Ukuaji wa haraka wa biashara na kuipanua sana au kuliko pindukia bila maandalizi
Ni jambo jema biashara inapokuwa na hivyo kujitanua kimasoko. Kuitanua sana biashara hadi kujikuta unaingia katika changamoto ya usimamizi bila maandalizi ni kuihatarisha biashara. Tangaza unachoweza kuhudumia

■=>Njia ya kukabiliana na hili
Epuka kuikuza biashara bila maandalizi. Jenga msingi imara wa kuhakikisha biashara inakuwa kwa utaratibu mzuri ambao utaweza kuusimamia kwa wepesi zaidi.

Hizi ni baadhi na wengine naamini bado wanaweza kuongeza katika kuboresha andiko letu na vilevile tujitahidi kutoa changamoto na namna gani mjasiriamali anaweza kutatua changamoto hiyo
 
Uko sawa
 
Service should stand as an input and profit should stand as an out put.Biashara nyingi zinakufa kwa sababu ya huduma mbovu utakuta siku za kwanza biashara ikiwa inaanza/mpya huduma zinakuwa bora hata care inakuwa ya hari ya juu.Lakini ikifika kipindi fulani owner/mwendeshaji anajenga mazoea hivyo hajali huduma bora
 
Back
Top Bottom