Kwa nini DPP angoma kumsomea Mshtakiwa shtaka lake?

mahirtwahir

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2013
Posts
613
Reaction score
313
Nimeshangwazwa na DPP kumsomea mshtakiwa shtaka lake baada ya kupanda kizimbani sikujua ni kipi kimemfanya asimsomee shtaka na kumuacha tena mtuhumiwa kuenda rumande.

Story iko hivi:-

Rafiki yangu alikua na mwanamke wanapendana sana mwanamme alienda kumposa (kumchumbia) ila mama wa mwanamke alikataa na kusababisha kuzirejesha pesa za mahari kwa familia ya kiume.

Mapenzi ya wawili hao hayakuvunjika yaliendelea siku ya tarehe 22/01/2019 mwanaume alimchukua mwanamke na wakaenda wanakokujua kwa ajili ya kuagana kwani mwanaume alikua anasafiri kwenda mbali kidogo kibiashara.

Baada ya kurudi mwanamke kwao aliulizwa kua ulikua wapia akasema ametoka kwa yule mwanaume maka ake alikasirika sana siku ya 23/01/2019 alimchukua mwanawe na kuenda kufungua jalada Polisi la kutoroshwa mtoto wake na kubakwa.
Mtoto alikataa kua hakubakwa ila mama alishikilia msimamo huo na kuenda kumpeleka hospitali kwa ajili ya kufanyiwa vipimo.

18/02/2019 alirudi mwanaume kutoka safari na kukuta taaarifa kutoka kwa mchukba wake kua "mama amenipeleka polisi na ameshashtaki kua umenibaka"

Basi mwanaume aliamua kuwatuma wazazi wake na kuenda kuomba suluhu basi mambo yamefanikiwa wakakubaliana kua waozeshe wawili hao wakafunga ndoa wawili hao 15/04/2019 ndoa ikafanyika.

Baada ya ndoa wameanza maisha yao ya furaha siku ya tarehe 2/05/2019 mwanaume alikuja kuchukuliwa kwake na kupelekwa polisi siku ilioguata alipandishwa mahakama ya wilaya ila hakusomewa shtaka lake kwani mahakama hio haikua na uwezo wa kusikiliza shauri hilo na walimpeleka rumande na tarehe 23/05/2019 alipamdishwa mahakama ya mkoa ila hakusomewa shtaka na DPP alikataa kata kata bila ya kutoa sababu ya kutosoma shtaka hilo.

Sasa jeee kwa nini na haki ipi inayomfanya DPP asisome kesi
Jeee kesi hio inaweza kupata zamana
Baada ya kufika mahakamani kesi ya kutorosha, kubaka ama kuomuondoa msichana chini ya wazazi wake liba dhamana hasa ukizingatia familia ishapitisha suluhi
 
Lawlessness Tanzania society!
 
Legal Aid Providers needed extensively
 
Daa aisee ,Watanzania ni wapumbavu sana,tunaendesha maisha kwa mhemko bila kufikiria athari zake,

Nampa pole sana jamaa

Binti alikuwa na miaka mingapi?
 
Daa aisee ,Watanzania ni wapumbavu sana,tunaendesha maisha kwa mhemko bila kufikiria athari zake,

Nampa pole sana jamaa

Binti alikuwa na miaka mingapi?
Miaka 19
 
Si kweli sheria ni "rushwa". Nitasimulizi alinifanyia nini Mkurugenzi wa DPP Ibrahim Mzee wa Zanzibar.
Siwezi kufikiri kwamba polisi huko Zanzibar hawataki kufanya kazi.
Askari DCI Mabakila anasinzia wakati nilipokuwa ninamweleza kesi yangu!
Mimi ni mzungu, nilidanganywa na nimeibwa na mwanamke anayeitwa SAM ambaye sasa anajaribu kuniibia kiwanja changu.
Mwanzoni aliniibia yuro 2000. Nilitoa ripoti katika kituo cha Mgambo. Hawakufanya kitu!
Nilitoa ripoti tena katika kituo cha Madema. Tena hawakufanya kitu!
Nilikwenda DPP nikaongea na Mkurugenzi Ibrahim Mzee lakini bila kufanikiwa alinidanganya tu! Mwisho mwezi wa mei wa mwaka jana (2018) aliniambia kwamba katika wiki moja tu angetuita ili tueleze mambo yetu. Wiki bado haukuisha!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…