Nimepata uhakika elimu bure inawezekana baada ya kumsikiliza Dr. Slaa. Kama JK anaweza kusambaza picha zake nchi nzima kwenye nyumba za maskini zilizoezekwa kwa nyasi, kwa nini Dr. Slaa asiweze kusambaza elimu bure kuanzia chekechea hadi kidato cha sita nchi nzima?
Kwanza pesa kusambaza za kusambaza sura yake kwenye mabango nchi nzima zimepatikania wapi?
Mkuu vitaje vyanzo vyz elimu bure ili watu waelewe kuwa siyo pesa iliyotumika kusambaza mabango ya JK kwenye nyumba za nyasi ingeweza kusambaza elimu bure nchi nzima bali Dr Slaa atatumia vyanzo vingine pia. Mkuu vitaje, tunafanya windo shopingi. Eleza wazi, watu wajue hili linawezekana kuanzia tarehe Dr. Slaa anayoapishwa kuwa rais na kuwekwa sawasawa katika muhula mpya wa masomo wa kuanzia tarehe 1.1.2011.
Mkuu, according to Dr. Kitila Mkumbo (Phd) katika kipindi cha tuongee asubuhi cha startv jana asubuhi ni kwamba;
Gharama za uendeshaji wa shule za msingi na sekondari including na tuition fees kwa mwaka ni shilingi takribani shilingi bilioni 100.
Akaeleza kuwa, kwa mujibu wa ripoti ya CAG, mwaka jana serikali ilitoa misamaha ya kodi inayofikia kiasi cha shilingi bilioni 700 ambayo ni kutokana na serikali kutoa msamaha wa kodi wa 2.7% kiwango ambacho ni kikubwa sana tofauti na nchi nyengine na kinyume na ushauri wa TRA kwamba serikali ipunguze misamaha hadi 1% ambacho ndio kiwango wanachosamehe wengine huko duniani.
Kama serikali ingefuata ushauri wa TRA, basi kiasi cha shilingi bilioni 500 kingeweza kuokolewa na hivyo tukapata bilioni 100 kugharimia elimu ya lazima ya kidato cha sita kwa kila mtanzania na tukabakiwa na chenchi ya bilioni 400 zikaelekezwa kwenye huduma nyengine.
Kwahiyo elimu ya lazima ya kidato cha sita inawezekana, afya bure inawezekana na makazi bora kwa kila mtanzania yanawezekana chini ya Chadema na Dr.Slaa(Phd).
Halafu mbona anasa zote za CCM hazijawahi kukosekana, ila pesa ya elimu na afya tu ndo iwe haitekelezeki!
basi tu kwa vile ni sisi Tanznia. lakini ingekuwa wenzetu CCM ishakuwa chali longiiiiiii!
wewe mpaka waongeze ukubwa wa serikali (yaani wakuu wa mikoa, wilaya) hatuna hela kweli, ufisadi wote wanaofanya!
Elimu bure inawezekana sana tu, na ndo maana wanmwogopa sana Dr. Slaa maana anasema ukweli