hapo kwenye bold, nadhani unaikimbia homework yako kaka.
ni kweli inamkera kila mtu, kusema ni laana pekee, haitoshi, labda utuambie nani alimlaani nani hadi matusi yanayoaminika kuwa makali na ya kuudhi zaidi yakaelemea huko kwenye kiungo cha mama. hata kusema wote tulipita hapo haitoshi, najua wengine hasa waliozaliwa kwa mikasi ya upasuaji hawakupita. labda ungetumia maziwa ambayo wengi wamenyonya, ila pia wengine hasa waliopoteza wazazi wakati wa kuzalia hawakunyonya nk. lakini hata kwa hayo bado uatakuwa umekimbia homework yako. pia kumbuka kuwa tusi ni socially defined na linategemea hisia za atukanae na atukanwae
umedadisi sababu na inakuwaje na maoni ndio kama hivyo kuwa source ya haya matusi kumuelemea mama yaweza kutazamwa kiantropolojia zaidi na hapo hutakwepa suala la fermine sensitivity.
fikiria hivi, kati ya mwanume na mwanamke, nani sensitive zaidi ya mwingine, ukipata jibu mwnamke, jiulize tena hivi, katika mwili wa mwanamke ni sehemu gani sensitive kuliko nyingine, halafu jiulize tena katika wanawake wote nani sensitive zaidi kwako ukipata jibu kuwa ni mama yako, basi hutoshindwa kuelewa how sacred is this organ, hasa iliyo kwenye mwili wa mama yako na kwa nini ntu anayetaka kukudhi atakutukania hilo.
ni kama vile mtu anayekufuru dini fulani ili kuwaudhi waamini wa dini ile, hupenda zaidi kukufuru fundisho kuu la imani na sensitive ya dini nyingine na sio mafundisho madogo madogo
haya mambo yana mizizi yake katika saikolojia na hayakutokea kwa nasibu bali yametokana na mchakato wa kiantropolojia
nafikiri sasa umenielewa.
Glory to God