Gosbertgoodluck
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 2,855
- 402
Jamani kama kuna jambo linalonikera basi ni hii tabia ya kutumia majina ya viungo nyeti vya wanawake kutukana. Utakia mtu bila aibu mbele ya hadhara anamtukana mwenzie eti k.... mamako. Ajabu ni kwamba kuna wakati nilimsikia dada fulani akimtusi mvulana kwa tusi hilo hilo!! Hivi ni kwa nini tunawadharirisha mama zetu kiasi hiki!? Kwa kweli hii ni laana tena laana kubwa sana!
ni kweli inakera. nafikiri wanatumia viungo vya mama kutokana na sensitivity yake. ikitokea mwanamke na mwanaume wanatemea uchi, ni most likely kuwa kwa mwanamke watu watakuwa sensitive zaidi. ndio maana hata mwanaume atembee kifua na mapaja yote nje, hutasikia mtu anatia neno, ila iwe hivyo kwa mwanmke, utasikia hata watu wakisema "ana laana huyu"!
kwa kuwa tusi ni neno linalotamkwa kwa lengo la kuudhi au kuumiza roho, basi atukanaye huchgua hapo kwenye viungo vya wakina mama kwani ndipo sensitive zaidi na mtu yoyote anayejiheshimu na kumheshimu mama yake hataweza kuvumilia si tu kuona, kushika nk kiungo cha mama yake, bali hata kusikia kikitajwa. nafikiri hata daktari akijikuta anatakiwa kumtibu mama yake sehemu hizo, itabidi kutafuta msaada wa daktari mwingine
Glory to God
kwa hilo nakubaliana nawe, pili maumbile ya mwanamke na ya mwanaume hayafanani kwa mvuto! Tumeona maumbile mengi ya wanawake na wanaume ukitukanwa kwa kiungo cha mwanamke then uvute picha ilivyo lazma utaghadhibika tofauta na yakiume!
:A S 13::crazy:K...mamake walahi hata mimi hiki kitu kinanikela sana
Mimi bado nafikiri kuwa hiyo ni laana tu. Kimsingi, hakuna binadamu ambaye hajazaliwa na Mama. Hata Bwana na Mwokozi Yesu Kristo alizaliwa na Mama. Sasa inakuwaje lile eneo tulilopita sote wakati wa kuzaliwa litumike kama tusi la kumuudhi mwenzio!! Wanadamu tumefika mahali tunakejeli uumbaji mtakatifu wa Mungu!! Ndiyo maana magonjwa hatari yanaendelea kutugaragaza na tusipobadilika tutaangamia kabisa.
hapo kwenye bold, nadhani unaikimbia homework yako kaka.
ni kweli inamkera kila mtu, kusema ni laana pekee, haitoshi, labda utuambie nani alimlaani nani hadi matusi yanayoaminika kuwa makali na ya kuudhi zaidi yakaelemea huko kwenye kiungo cha mama. hata kusema wote tulipita hapo haitoshi, najua wengine hasa waliozaliwa kwa mikasi ya upasuaji hawakupita. labda ungetumia maziwa ambayo wengi wamenyonya, ila pia wengine hasa waliopoteza wazazi wakati wa kuzalia hawakunyonya nk. lakini hata kwa hayo bado uatakuwa umekimbia homework yako. pia kumbuka kuwa tusi ni socially defined na linategemea hisia za atukanae na atukanwae
umedadisi sababu na inakuwaje na maoni ndio kama hivyo kuwa source ya haya matusi kumuelemea mama yaweza kutazamwa kiantropolojia zaidi na hapo hutakwepa suala la fermine sensitivity.
fikiria hivi, kati ya mwanume na mwanamke, nani sensitive zaidi ya mwingine, ukipata jibu mwnamke, jiulize tena hivi, katika mwili wa mwanamke ni sehemu gani sensitive kuliko nyingine, halafu jiulize tena katika wanawake wote nani sensitive zaidi kwako ukipata jibu kuwa ni mama yako, basi hutoshindwa kuelewa how sacred is this organ, hasa iliyo kwenye mwili wa mama yako na kwa nini ntu anayetaka kukudhi atakutukania hilo.
ni kama vile mtu anayekufuru dini fulani ili kuwaudhi waamini wa dini ile, hupenda zaidi kukufuru fundisho kuu la imani na sensitive ya dini nyingine na sio mafundisho madogo madogo
haya mambo yana mizizi yake katika saikolojia na hayakutokea kwa nasibu bali yametokana na mchakato wa kiantropolojia
nafikiri sasa umenielewa.