Kwa nini hatujakuza utalii wa 'kuuona mwaka mpya mapema'?

Kwa nini hatujakuza utalii wa 'kuuona mwaka mpya mapema'?

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Kuna aina nyingi sana za utalii. Mwingine unatokana na asili ya eneo husika, historia, utamaduni, nk.

Dunia ya leo, utalii wa kisasa unatumia asili ya eneo husika na unaliongezea thamani kwa kutengeneza unique experience kwa mtalii anayekuja.

Tanzania tumebahatika kuwa eneo kigeographia ambalo tuko masaa kadhaa mbele kulinganisha na miji mingi ikiweko ile mikubwa duniani. Hii inatufanya tuwe na unique advantage ya kuuona mwaka mpya mapema kabla ya nchi nyingi duniani, ikiwemo zile tajiri kabisa.

Hili linaweza kuonekana jambo dogo kwa sababu hatujajua thamani zetu. Kila mwaka tunauona mwaka mpya masaa 3 kabla ya yule aliyeko London, masaa 8 kabla ya yule aliyeko New York, na masaa 11 kabla ya yule aliyeko Los Angeles, California. Ila miji inayojulikana kwa sherehe za mwaka mpya ni kama New York.

Imagine kama mwaka mpya ungekuwa unaanzia New York au Los Angeles, tungeona jinsi wanavyojibrand na movie kadhaa za Hollywood zingetengenezwa kutukumbusha hilo na kwa jinsi gani miji mingine ni 'inferior'.
 
Back
Top Bottom