SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Ukiwa na aibu kuna mambo fulani utajizuia kufanya mbele za watu hata kama unatamani sana na una haki ya kuyafanya.
Miaka hii miwili matatu tunaona wimbi la watu kutoka Simba kuelekea Yanga kwa kurubuniwa na Rais wao aliyekataliwa na mahakama Hersi Said. Imekuwa kama lile wimbi la "waunga mkono juhudi" enzi zile.
Tukianza kutoa mifano, haikuleta maana kwa Yanga kumrudisha Morrison kipindi kile ila alirudi na mwisho wa msimu ikaonekana haukuwa uamuzi mzuri sana ingawa mimi naamini goli lake kwenye CAFCL lilichangia sana Yanga kuvuka hatua inayofuata.
Tukaja kwa Haji Manara. Ni kwenye siasa zetu pekee ndiyo unaweza kukuta kile tulichokiona kwa Manara. Aliikandia sana Yanga, walipata kila aina ya kejeli ila alipoondoka Simba, tukashangaa amepokelewa upande wa pili.
Msimu uliopita akamleta Augustine Okrah pamoja kujua sababu zilizomuondoa Simba. Matokeo yake Okrah akapotea mazima na sijui kama alicheza hata mechi 5.
Tumefika kwa Clatous Chama. Huyu amemtamani kitambo sana na nafikiri msimu huu hata asiposhinda chochote, kitendo tu cha kumpata Chama ni kama anajiona ameshatimiza ndoto zake. Nimeangalia interview yake kule Afrika Kusini, kajisifu sana kumsajili Chama.
Kuna Baleke. Huyu naona kama wanagwaya kutamba naye ndiyo maana mpaka leo utambulisho rasmi haujaja.
Nasikia Kibu naye huyooo inasemekana anaenda vyurani. Huyu Kibu alipokuwa Mbeya City, Yanga walimteka ili kumsajili akawatoroka akaenda kusajili Simba na kwa maneno ya Kibu mwenyewe Hersi ndiyo alikuwa injinia wa zoezi zima la kutekwa kwake, pun intended. Inaonyesha hii ilibaki kuwa ndoto ya Hersi kuwa na Kibu.
Na kuna watu wengine wakiwemo viongozi ambao ninafahamu Hersi ameshawahi kujaribu kuwavuta upande wa pili. Kwa wachezaji waliobaki naamini kuna siku atamvuta Mohamed Hussein Zimbwe. Ni suala la muda kabla hatujamsikia Aubin Kramo na Moses Phiri upande ule. Pia sitashangaa kama siku moja hatamchukua Miqssone.
Hii obssession kwa watu wa Simba inasababishwa na nini? Kama anadhani ataibomoa Simba kwa njia hii nadhani anapoteza muda wake na pesa za klabu. Apunguze mapenzi binafsi yaliyojificha kwa Simba, ajue Wazee wa Yanga wanasubiri tu siku yoyote watekeleze amri ya mahakama.
EDIT: Nilimsahau na Jonas Mkude. Huyu alitambulishwa kwa mbwembwe zote kama vile kinda atakayeenda kutikisa nyanja za soka kwa miaka 20 ijayo....