Hehehehehe. . . huu ni ugonjwa?
Nwy ngoja nijaribu kuilezea kwa mtazamo wa kisaikolojia ili jibu liendane na jukwaa husika.
Kwenye saikolojia kuna kitu kinaita Conformity. Hicho ni kitendo cha mtu kubadilika kifikra, kimuonekano, kitabia n.k ili aendane na mazingira yanayomkabili au wakati mwingine anafanya hivyo ili tu atimize hitaji lake la kuwa KUNDINI badala ya nje ya kundi. Yani nae afanane na wenzake, asionekane tofauti/mshamba/asiyejua kitu.
Mf. Mzuri ni asilimia kubwa ya vijana wanapoanza kuvuta sigara/kunywa pombe. Wengi hua wanaanza kufanya hayo kwasababu marafiki zao wanafanya hayo. Kukwepa kuitwa mshamba ama kuonekana mjuaji/wa ajabu kwa kutofanya kitu ambacho ni cha kijinga ila kinachokubaliwa na kundi.
Nikirudi kwa wadada na lafudhi vs wakaka na lafudhi.
Kwa wadada kujionyesha nae ni wa mjini ni muhimu kuliko kwa wakaka. Hao mabinti wanapokuja mjini wanaona hitaji la wao kufanana na waliowakuta ili nao wafanane na waliowakuta pia wasiitwe/wasionekane ni washamba, kitu ambacho hakiwasumbua sana vijana wa kiume.