Elections 2010 Kwa nini hofu ya upadre wa Dr. Slaa haina msingi

  • Thread starter Thread starter PJ
  • Start date Start date
Kama mtu alidokoa nyama miaka mitano iliyopita then last year hakudokoa kwangu mimi kwenye file lake naandika ana tabia ya udokozi.Sasa Slaa wenu ni kigeugeu.That's it.

Kumbe kadokoa nyama miaka mitano iliyopita bado unakumbuka hilo. Mbona sasa unasahau haraka wanaodokoa hata sasa? Au kwa vile ni wengi na akili yako ni ndogo hivyo sio rahisi kuwashika wote hawa wa sasa, ukabaki na huyo wa zamani ambapo akili yako bado ilikuwa inashika. Sasa kama una akili ndogo kiasi hicho kwanini ujiingize kwenye mijadala mikubwa? Sio lazima ujadili wewe kama huna uwezo nao.
 
CCM imeshindwq kutunza ahadi ya kuwaletea maendeleo waTZ kwa maiaka 50 sasa, thats is more important kuliko maisha ya mtu mmoja. They are the ones who should go.
 
Tunapofuata mambo madogo madogo ya unyumba wa mtu binafsi kwa gharama ya mambo makubwa ya taifa ndipo tunapokosa mwelekeo na kubaki tukirudi nyuma wakati majirani zetu wakizidi kusonga mbele. Dr. Slaa alikuwa padri kwa miaka kama 14 hivi tangu mwaka 1977 hadi mwaka 1991, halafu akawa mbunge kwa 15 tangu mwaka 1995 hadi mwaka 2010. Ni jambo gani tusilojua kuhusu jamaa huyu linalotufanya tutumie nguvu nyingi kutafuta kama ni padri au siyo padri? Kwa nini basi tusisema kuwa ni mbunge wa Karatu anayemaliza muda wake amaboyo ni nafasi yake ya hivi karibuni zaidi kuliko kuangalia kazi aliyofanya miaka karibu ishirini iliyopita? Kama kazi aliyofanya miaka ishirini iliyopita inazidi umuhimu kazi aliyofanya miaka kumi na tano iliyopita basi kuna wanasiasa wengi Tanzania hawatakuwa na sifa za kuongoza kwa vile baadhi yao walikuwa hawajatimiza umri unaotakiwa au walikuwa bado mashuleni, wengine walikuwa ni wanajeshi, na wengine walikuwa ni wababaishaji wa mitaani tu.

Let us be serious

Kama kazi yake aliyofanya kama mtumishi wa dini yake ndilo tatizo kubwa linalopigiwa kampeini ya kisisas sasa, basi hata wafuasi wote wa dini aliyowahi kutumikia hawana sifa za kuingoza Tanzania, kwa hiyo wakatoliki wote siyo sehemu ya taifa hili.

Where are we heading to?
 

Unamuamini wewe na wale wachache waliompiga Makenji kule Kinondoni.
Na kama unaamini hivyo,si wote tunaamini hivyo.
How do I trust a man who can't keep his promises or vows???
The best part of the show's he won't win.(Am sure he knows it though anajua pia wapo watu kama ninyi with your way of thinking).
 

You are so fun! huwezi kumuamini Dr. Slaa cause he can't keep his promises or Vows! hahaah very fun, yet you trust Kikwete ambaye ameshindwa ku keep promise yake as well, hebu tuambie ni mtanzania gani zaidi ya MAFISADI wa CCM aliyepata MAISHA BORA kama alivyo ahidi JK! You know what, ninafuraha sana baada ya kugundua kumbe hata watanzania wa hali ya chini sana ( wasukuma guta) sasa wameisha gundua kuwa JK is a joker! Kama uliangalia kipindi cha USWAZI cha Chanel 5 (EATV) jana jioni basi unaweza kuwa na jibu!
 

Pumba!
 

nadhani kama hawa watu wangeumia nguvu nyingi namna hii kuelewa ubaya wa mafisadi ningewasifu na ubaya wa kusaini mikataba hotelini nje nchi mbona maendeleo yangekuja kwa speed ya ajabu

jamani watanzania wenzangu tujifunze kuacha kupoteza muda na kuweka mada ambazo zipo nje ya mtizamo mpana wenye tija
 
Mhhh!!! Kampeni mwaka huu zaenda kusiko kabisa!! Sababu yake? Just say it....CCM maji marefu this time....mtajibeba tu hata mlete mambo chungu nzima yasiyohusu, wananchi wameamua kuitosa CCM. Hivi huyo JK wenu akipigwa darubini kali mtaona nini? Si uchafu.... na uchafu.... na uchafu.... na uchafu.....!!!! Turudi kwenye mada za msingi, kama nyie kweli ni wanaume!
 

Kwangu dole tu nakupa, Mkuu Zak. Kwani vita ya madongo na uchafu CCM hawataiweza kamwe kwa machafu yao yaliyokithiri.. na ndo maana wakiguswa tu -- eti ooh "matusi".
 


Kwanza karibu jamvini halafu asijui baada ya uchaguzi utaondoka au utabaki!

Hapo kwenye red inaelekea mmna amini kila anachosema JK maana huyo ndio anayejua ku -keep promises like mabasi yaendayo kasi tangu uchaguzi wa 2005 hadi leo hayajaonekana sasa kaja na flyover sijui ataziweka wapi ikiwa ule mradi wa mabasi umemshinda??? SHAME ON YOU AND OTHER CCM. Unaacha kujadili mambo ya msingi unajadili UDINI.

Kumbuka WATANZANIA WANATAKA KIONGOZI ANAYEJALI MASLAHI YAO NA ANAEOGOPA KUHUJUMU NCHI IKIWEMO UFISADI, KUJILIMBIKIZIA MALI. HATA MWL NYERERE (RIP) ALISEMA KIONGOZI BORA LAZIMA AWE MCHA MUNGU ILA HATUTAMCHAGUA KWASABABU YA KABILA,RANGI WALA DINI! Upo hapo ndugu yangu
 
CCM imeshindwq kutunza ahadi ya kuwaletea maendeleo waTZ kwa maiaka 50 sasa, thats is more important kuliko maisha ya mtu mmoja. They are the ones who should go.

Kuwaletea maisha bora???????Ndo slogan ilivyo???
 
Exactly.Sakramenti ya upadre katika kanisa katoliki ni lifetime thing.Wasituongopee hawa mabwana.

Hudanganywi ukweli wenyewe ndo huo ulioelezwa labda kama ubishe tuuu!!!
 

padri anaweza kuwa rais wa nchi hata kama bado ni padri katika nchi zenye wachristo wengi na ni lazima nchi hio iwe ya kidemocrasia kweli sio tanzania.
Dr. Slaa anaweza kuwa ni kiongozi mzuri ndani ya kanisa , na bungeni ameonesha uhodari wa kupasua mabomu ama scandal bungeni ..

Pengine hii ilikua ni njia ya kutafuta umaarufu ili kuja kugombea urais. Sio sifa inayotosha kuwashawishi watu wamuamini hasa ikizingatiwa chadema ni chama kichanga sana.

Suali jee kama padri anaweza kuwa rais wa nchi hii ?? Jawabu abaweza katiba haimkatazi...lakini jee raia wa nchi hii wanamwamini kumpa kura zao ?
Jawabu sio rahisi....kwa nini ??? Kwa sababu nchii hii tayari kuna mgawanyiko mkubwa wa kidini ..kila mtu anavutia upande wake ki-maslahi...japo hakuna mfarakano...wa magomvi lakini hakuna kuaminiana huu ndio ukweli....hivyo sio rahisi upande wa waislam kumpa kura mtu ambae amewahi kuwa padre.....hasa wa kikatoliki.....mtakumbuka waislamu namna gani wanavolalama kwamba wakati wa nyerere mapadri walipendelewa tena hasa wa kikatoliki....maandishi yao yapo na ushahidi wao upo...hivyo sio rahisi kumwamini dr slaa hata kidogo...kura zao ni muhimu sana kumweka mtu yoyoyte ikulu...

Ni hivyo hivyo kama sheikh mussa kundecha ange gombea urais ....wakristo wangekua na mashaka nae...na magazeti na hapa jf....angepewa majina kama ..mujahidina....

So slaa anaweza kuwa rais katiba inamruhusu....lakini kama urais unaupata kwa kura...na kura za nchii hiii zimegawika baina ya wana dini wa 2 basi upande mmoja sio rahisi kumwamini....hakuna ushahidi ama hajawahi kuonesha kuwapo pamoja na waislam..kwenye sehemu zao ama hata kuwatakia salam tu za eid au ramadhan amejitenfa nao tangu amekua padri mpaka katika pirika zake za ki siasa....haoneshi kama ni kiongozi wa wote...



 
Mwizi wewe unayetaka mtu apate popularity isiyo na msingi wakati naye ni tatizo tu.Mbona alilamba marupurupu ya ubunge??Si alilalama yalikuwa makubwa??Angeyakata basi.

Kuna mapadri wangapi wameoa na wanaendelea na maisha yao kama kawaida, kuna mapadri wangapi wangapi bado wako kwenye service na wamezaa watoto mitaani licha ya kiapo unachokifagilia. Suala la kutumika katika kazi ya Bwana ni suala binafsi wala hakuna kifungu kwenye bible kinachokataza watu kuoa kwa ajili ya kumtumikia Mungu.

Siwezi kum judge mtu kupitia maisha yake binafsi. Huyo Mkwere anao watoto wangapi wa mtaani?and that doesn't bother me at all as long as He is doing job correctly! Wapo akina Zuma wa Afrika ya kusini, Bill clinton na Ronald Regan waliowahi kuhusishwa na masuala ya wanawake wakiwa madarakani, je hilo liliathiri ufani na utendaji wao kazi? La Hasha!

CCM wamekosa cha kumkosoa kuhusia na utendaji na record zake, wameanza ku-attack personal life! His record is clean and He has been consistent and with what He preaches despite of several attempts to bribe and silence Him.
Kinachoniumiza zadi ni watu kama nyie mnaodhani siku moja CCM iliyoshindwa kuleta maendeleo licha ya miaka 50 ya uhuru itakuja badilika! Never hilo sahau! Hakuja cha majaaliwa future is in your hand! Umeridhika na tunavyoibiwa sio? Nina kuhurumia! Si ajabu umeenda shule na uko wapi utashi wako wa kuuliza na kuhoji mambo yasiyoenda sawa! Cheo ni dhamana na nitakuwa tayari kumhoji yeyote atayeingia madarakani maana ni haki yangu ya msingi!
Endelea kusubiria majaaliwa!
 
Kuwaletea maisha bora???????Ndo slogan ilivyo???
Maisha bora imeshindwa kuyaleta ktk miaka 50, halafu inaomba kuyaleta maisha bora TENA kwene miaka 5 ijayo..lol..Hata mtoto mdogo hawezi kukubali huu upupu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…