Kwa nini ikitokea visa vya mauaji Zanzibar wahusika ni watanganyika?

Kwa nini ikitokea visa vya mauaji Zanzibar wahusika ni watanganyika?

aleesha

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
798
Reaction score
1,178
KIJANA mmoja alietambulikana kwa jina la Noel Jengeni Mlilo mwenye umri 27, mkazi wa shehia ya Wawi wilaya ya Chakechake, na mwenyeji wa Mkoa wa Songwe Tanzania bara, amekutikana kichakani akiwa amefariki, shehia ya Mtuhaliwa wilaya ya Mkoani Pemba.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kaka wa marehemu huyo, Devista Jengeni Mlilo (30), alisema marehemu aliondoka nyumbani kwao tokea Oktoba 12, na hakurudi siku hiyo na siku iliyofata wakaanza kutoa taarifa katika vituo vya Polisi Mtambile na Mkoani kwa ajili ya kupata msaada wa kumtafuta ndugu yao.

Alieleza, ndugu yake hakuwa na matatizo yoyote ya akili, alikuwa akifanya biashara zake hasa eneo la Mkoani, ingawa baada ya kutorudi na kumkosa kwa simu, walilazimika kufika vituoni kutaka msaada zaidi.

Mashuhuda wa tukio hilo, Zakaria Mgeni na Omar Shora, walisema wakiwa kwenye shughuli zao za kawaida, waliuona mwili wa marehemu karibu na shina la Muembe ambapo baadae waliamua kutoa taarifa kwa wananchi wengine wa Mtuhaliwa.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa mwili wa marehemu uliofanywa na jopo la madaktari akiwemo daktari Mohamed Faki Saleh, alisema marehemu alikuwa na majeraha madogo madogo sehemu za mbele za mwili wake na mgongoni alikuwa na jeraha ambalo lililoonesha kusababishwa na kitu chenye ncha kali.

Alifafanua, hiyo inaweza kuwa sababu moja ya kifo cha marehemu, na nyingine ni kukosa hewa aina ya oxgen na kuachana kwa mifupa ambayo yalisababishwa na mkabo uliokusudiwa kutenganishwaa kwa kichwa na kiwiliwili .

“Marehemu anaishara kama aliekabwa na inaonekana waliofanya hivyo, walikuwa na lengo la kutengenesha kichwa na kiwili wili, maana ana alama kubwa, lakini hawakufanikiwa, ingawa walimkosesha hewa na kisha kufariki,’’alifafanua daktari huyo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa kusini Pemba, Hassan Nassir Ali alisema taarifa hizo walizipokea majira ya saa 2:30 asubuhi kutoka kwa ndugu na jamaa wa marehemu.

“Kwa sasa tunaanza upelelezi wa kina ili kujua ni nani aliehusika na tukio hilo, ambalo lina kila dalili kuwa wapo watu waliojichukulia sheria mikononi mwao, na sisi tunawatafuta,’’alifafanua.

Mwili wa marehemu huyo, ulikabidhiwa kwa ndungu zake kwa ajili ya mazishi.

Hili ni tukio la pili kwa mwaka huu kwa Mkoa wa Kusini Pemba, kuokotwa mtu akiwa ameshafariki, ambapo la mwanzo ni lile la August 1, ambapo iliokotwa maiti ikiwa imeshaoza eneo la shehia ya Wawi wilaya ya Chakechake Pemba.
 
Wakina Makame kwa asili ni watu kutoka Tanganyika.

Ukifika hapa Zbr utakuta watani zangu wanyamwezi wamezaliana kiasi cha kutosha.
 
ehhhhh
hata wale waliokuwa wanamwagia watalii tindikali walikuwa watanganyika........
wale masheikh nao ni watanganyika.
vitendo vya kiovu haviusiani na asili ya mtu. yoyote yule anaweza kufanya anaweza mkuwa mtanganyika au mzanziberi.
 
Binti point yako nini haswa,mbona hauliizi Kwa nini kila shoga Zanzibar ni mzanzibar asilia?
 
ehhhhh
hata wale waliokuwa wanamwagia watalii tindikali walikuwa watanganyika........
wale masheikh nao ni watanganyika.
vitendo vya kiovu haviusiani na asili ya mtu. yoyote yule anaweza kufanya anaweza mkuwa mtanganyika au mzanziberi.
Naona wenyewe wamekuja juu
 
kupatikanika na kutikanika sio kiswahili,mwambie na mwenzio evans mhando wa tbc1
 
Uzi unatia kichefuchefu, kichwa chengine na maudhui mengine. Unaamsha ari ya mjadala wa kibaguzi kiasi fulani. Ila uovu hauna ubaguzi huweza kutendwa na yoyote haijalishi kabila, dini, eneo au asili ya muovu.
 
Back
Top Bottom