Zamani kulikuwa hakuna magonjwa, chakula kilikuwa kingi, elimu ilikuwa bure na hata kuishi watu walikuwa wanaishi maisha marefu kuliko sasa. Sasa hv ukibeba mimba ukizaa salama ushukuru mungu unaweza ukabeba mimba ukaumwa sana mpaka uctamani kubeba nyingine, au ukabeba mimba wakati wa kujifungua ukala kisu na mtoto ukakosa (na hii sasa inawatokea watu wengi sana cjui ni kwa nini). Hata elimu kwa sasa ni gharama kubwa sana c kwa masikini wala tajiri na kikubwa zaidi wote baba na mama wanakimbiza pesa na walezi wa watoto wanapatikana kwa tabu, kuwameintain ni gharama kubwa pia na hawakai sana kwa waajiri wao ni wepesi kudanganyika. Zamani ulikuwa unaweza kuomba ruhusa kazini ukakaa hata mwezi unaangalia watoto kama huna mlezi sasa hivi thubutu kama kibarua hakijaota mizizi na kikiota mizizi baba nae anaanza kukuona mzigo