hao wazamani kuwa na watoto wengi ilikua ufahari hawakujali watawatunzaje, sasa hebu imagn maisha ya sasa unaishi chumba kimoja uswahilini utazaa 10 uwalaze wapi? uwalishe nn? Kwa maisha ya sasa acha tu wazae wawili wanawatosha kabisa
Zamani kulikuwa hakuna magonjwa, chakula kilikuwa kingi, elimu ilikuwa bure na hata kuishi watu walikuwa wanaishi maisha marefu kuliko sasa. Sasa hv ukibeba mimba ukizaa salama ushukuru mungu unaweza ukabeba mimba ukaumwa sana mpaka uctamani kubeba nyingine, au ukabeba mimba wakati wa kujifungua ukala kisu na mtoto ukakosa (na hii sasa inawatokea watu wengi sana cjui ni kwa nini). Hata elimu kwa sasa ni gharama kubwa sana c kwa masikini wala tajiri na kikubwa zaidi wote baba na mama wanakimbiza pesa na walezi wa watoto wanapatikana kwa tabu, kuwameintain ni gharama kubwa pia na hawakai sana kwa waajiri wao ni wepesi kudanganyika. Zamani ulikuwa unaweza kuomba ruhusa kazini ukakaa hata mwezi unaangalia watoto kama huna mlezi sasa hivi thubutu kama kibarua hakijaota mizizi na kikiota mizizi baba nae anaanza kukuona mzigo
Yaani wapo wenye uwezo mkubwa na majumba yao na miradi mbali mbali wala hawafikirii saaana pa kuwalaza wala kuwalisha lakini wanaishia watoto 3 tena hata usiseme uswazi maana huko hata watano (5) wanazaa yaani Vice versa kwa hiyo sababu ya uswahilini na uchumi sijaona kama ya msingi maana matajiri ndiyo wanaongoza kwa idadi ndogo ya watoto wa 2 au 3
Hapo kwenye red ndipo nahitaji kupajua maana mmmmh
Matajiri wanaongoza kwa watoto wachache kwani hata matunzo ya watoto hao gharama zake hawezi kuzaa watoto wengi, shule wanazosoma chakula wanachokula, starehe wanazowapa na bado wenzetu matajiri wanawawekea akiba watoto wao ili hata ikitokea bahati mbaya wamekufa watoto wanakuwa angalau na pa kuanzia. Kwa hiyo wanazaa watoto wachache ili wawape malezi bora na si bora malezi
Hakuna anayeiga uzungu kwa kuzaa watoto wachache ni hali halisi. Kama unata uishi maisha waliyoishi baba zako zaa watoto wengi, tena sasa hivi mabadiliko ni mengi. Watoto wengi ni mzigo mkubwa usiobebeka. Sema wazungu walistukia mapema. Wenye kipato kikubwa ndo wanajua balaa la umaskini kuliko maskini wenyewe. Kwa hiyo wenye kipato siku zote wanafanya juu chini ili kipato chao kiendelee kuongezeka na si kupungua. Ukishapata kipato, kurudi kwenye umaskini ni sawa na kufa. Mojawapo ya mbinu ya wenye kipato kuhakikisha hawaanguki (au hata wakianguka waanguke vizuri) ni kudhibiti ukubwa wa familia.
Kwa hali ilivyo sasa hivi watoto wawili (replacement level) ni sahihi kabisa. Binadamu si mbwa au kuku. Lazima tupange. Zamani watu walikuwa wanakwambia wanazaa wengi ili wengine wakifa wengine wabaki. Siku hizi malezi ni bora, vifo vya watoto vimepungua mno. Ukizaa wawili uwezekano mkubwa ni watakua wote. Sasa hivi watu wanafikiria nikifa nitawaachaje wanangu! Ule ujinga wa kila mtoto anakuja na riziki yake unazidi kupungua kwani sasa tunajua riziki ya mtoto iko kwa wazazi wake!
Afadhali hukusome ualimu maana ningekuwa mwanafunzi wako ningetoka kapa ingawa ni jiniazi
jiniazi!!!!!!!!!!!!!!
jiniazi unaewaza kuzaa watoto wengi zama za leo
Ukianza kuzaa na miaka 35 utazaa mara ngapi kabla hujafikia au kukaribia menopause.
Yah hii inaweza kuwa mojawapo ya sababu za msingi maana enzi zile wasichana /. wanawake walikuwa wanaolewa katika umri mdogo sana na uwezo wa kuzaa watoto wengi ni mkubwa mpaka wafikiapo uzeeni
Mi nadhani ni kwenda na wakati wenyewe wanasema. Angalia mtu ana watoto wawili au mmoja na mkewe wa ndoa, lakini ana wengine 2-3 na vimada, sasa unajiuliza inakuwaje ???
Si kwamba ni ugumu wa maisha, na ndio hawa hawa wenye uwezo tunaosema.