Ndugu wana jamvi adhimu la Jamii Forums nawasalimu. Ama baada ya kuwasalimu mwenzenu nina pendekezo moja. Linahusu wazo la memba wote humu kuchangia kiasi Fulani cha pesa tukawapa moderators wetu na kisha kuzipeleka katika mradi wowote wa elimu. Hii itakuwa sehemu ya sisi wanajamvi kuchangia maendeleo ya elimu yetu. Kwa mfano, tunaweza kusema tuchangia buku kumi kumi kila mmoja kisha zipelekwe kununua madawati katika shule za msingi katika baadhi ya maeneo hapa nchini. Hilo ndilo pendekezo langu wakubwa