You know, watu wanaoa na wengine kuolewa kweli wanajua kwa nini wafanya jambo hilo? Wengine wanaweza kuoa kwa sababu wamewaona wenziwao au rafiki zao wanaoa au kuolewa, wengine tamaa ya tendo la ndoa nk Nilichotaka kufahamu ni: (1) Kama wewe umeshaoa/ kuolewa tayari au labda utaoa au kuolewa baadaye kwa nini umelifanya/ utalifanya jambo hilo. (2). Nilitaka kufahamu pia kama ni lengo la kuwa na msaidizi au mtu wa karibu kwa nini watu wengine wanaoa watu wa jinsia moja? Nia yangu ni kupanuana mawazo au kupeana elimu kuhusu swala la ndoa ambalo ni agizo la Mungu - Asanteni