vamda
JF-Expert Member
- Aug 1, 2012
- 895
- 571
Ndugu wana JF. Napenda kufahamu kwa nini maafisa elimu wengi waliokabidhiwa ofisi wilayani na kwenye miji hapenda kunyanyasa na kuwaonea walimu. Kwa mfano mwalimu anaweza kumpelekea barua ili aisaini, afisa huyo anaweza kukaa nayo ofisini hata miezi 2 bila ya kuisani tena bila ya sababu za msingi. Kwa nini walimu wamekuwa watu wa kuonewa hapa nchini tena na walimu wenzao (maafisa elimu) wenye ofisi?