DOKEZO Kwa nini Mamlaka zimekitelekeza Kituo cha Daladala Zingiziwa – Chanika?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Nyakijooga

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
524
Reaction score
829
Ukifika Chanika mwisho jijini Dar es Salaam kuna msongamano mkubwa wa magari na watu kutokana na ufinyu wa eneo hilo. Hiyo ni kwasababu eneo hilo halina kituo cha daladala, matokeo yake magari hayo hujichanganya na pikipiki zinazopaki eneo hilo na msongamano wa watu.

Msongamano huo ulisababisha kuanzishwa ujenzi wa Kituo cha daladala kilichopo eneo la Videte Kata ya Chanika umbali wa kilometa mbili kutoka Chanika. Hata hivyo, kituo tangu kianze kujengwa mwaka mmoja uliopita, hakijakamilika.

​
Baadhi ya madereva na majirani wanaoishi eneo hilo wamesema, waliambiwa kuwa kituo hicho kitaanza kutumika Oktoba 2025, lakini kituo hakijatumika mpaka leo.

Hata makondakta nao ukiuzungumza nao watakwambia walipewa stori hiyohiyo kuwa kituo kitaanza kutumika baada ya kuzinduliwa.

Pamoja na hivyo kuna Wananchi ambao nao wanadai Stendi hiyo ipo mbali tofauti wanadai kama abiria anashukia Chanika, utampeleke mpaka kule Videte? Wanadai kama abiria watashukia wote Chanika maana yake inakuwa haija haja tena ya kwenda kule stendi.

​
 
Inamaana hilo jengo jeupe ndo kituo chenyewe cha daladala?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…