Kwa nini mark za timingi ni muhimu

Kwa nini mark za timingi ni muhimu

INJECTION TECHNICIAN

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2020
Posts
356
Reaction score
794
HABARI WANA JAMVI NAOMBA TUJIFUNZE KITU MWENYE KUONGEZEA ASISITE KUTOA MCHANGO WAKE

Mark za timing ni kiashirio muhimu kinachotumiwa kuweka uwiano wa kuwasha injini. Kwa kawaida hupatikana kwenye puli ya crankshaft,camshaft au flywheel, inasaidia kuhakikisha kuwa injini inawaka kwa wakati muwafaka kwa utendakazi bora. Alama hizi huwekwa kwenye sehemu zinazozungushwa na crankshaft, pamoja na crankshaft yenyewe huwa na alama

Kwa nini mark za timingi ni muhimu:

Engine iliotegwa timing vizuri:hupelekea kuwaka vizuri na kwa wakati vile vile hufanya kazi kwa ufanisi

Huzuia muungurumo usio sahihi kwa Injini: timing isiyo sahihi inaweza kusababisha muungurumo usio sahihi na kusababisha injini kugonga gonga


Timing iliotegwa vizuri hupelekea Mafuta kuchomwa vizuri na kwa muda unaofaa

NI hayo tu
IMG_20241109_152019_811.jpg
 
Back
Top Bottom