Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 4,151
- 4,277
Swali kuu la uchumi ni chaguo mojawapo.Uzalishaji wowote wa kiuchumi unatawaliwa na muda pamoja na raslimali zilizopo ili kutumika.Lakini mahitaji ya watumiaji kula,kuvaa,kujenga na kupumzika kwa namna mbalimbali ni mahitaji yasiyo na ukomo.
Baadhi wanaweza kuridhika lakini vipi kuhusu wengine wasioridhika?Sharti machaguo yafanyiike kuhusu mahitaji yanayotakwa na wengi ili kuzalisha bidhaa au huduma hitajifu badala ya ilimradi.
Uchumi ni elimu ya kujifunza kuhusu swali kuu katika maisha juu ya uhaba na mwitikio wa binadamu juu yake.Ni ujifunzaji wa kufanya maamuzi.
Ni suala la muhimu sana kila mmoja wetu kujifunza au kufundishwa kufanya maamuzi katika ulimwengu wa vitendo (maisha ya kila siku).
Usimamizi wa nyumba,biashara,matumizi ya posho,au utawala wa taasisi yoyote ile unahusisha maamuzi ya kiuchumi.Chaguo ndiyo sifa kuu ya maisha ya kichumi.
Itaendelea...