Jioni baba mwenye nyumba anakuwa amesharudi, hivyo ni competition na mama mwenye chake.
Kwa mabinti wa kazi za ndani walivyo siku hizi hawajatulia, utanunua sare ngapi kwa mwaka? Siku hizi ukibahatika kukaa na binti miezi sita mhhh, hasa kama una watoto wadogo hawataki kabisa! Wamekuwa wasumbufu kiasi kwamba wazazi wameamua kupeleka watoto wao day care centres (at least sasa zipo chache japo ni fedha nyingi sasa inabidi ulipe tu). Nafikiri itafika mahali tutakuwa kama nchi za wenzetu, kuwa ni vema kumpeleka mwanao day care centre acheze na toys na kujifunza kuliko kubaki huko nyumbani akikoromewa na haouse girl ambaye pengine ni drop out na mbaya zaidi analetewa ma unlce ndani wanazini mbele ya mwanao. Nakumbuka enzi hizo watoto wangu walilelewa na wafanyakazi wawili tu (kabila langu) kwa nyakati tofauti kwa kuwa wote walipata wachumba na kuolewa wakitokea kwangu. Watoto wao ni kama ndugu maana mpaka leo wanafika kwetu (bahati nzuri waliolewa DSM na wana maisha mazuri mno, mmoja wana duka la jumla kubwa na mumewe -mtaji niliwapatia na wakautumia vizuri, tena kwa wakati huo ulikuwa mtaji mdogo ila kwa kuwa binti alionyesha interest ya biashara tangu nikiishi naye basi ikawa ndiyo zawadi yake wakati wa ndoa yake, mwingine nilimsomesha tailoring school -ndicho alichoweza, na akawa na tailoring mart/ school registered by VETA na sasa ana duka la nguo na ni mteja Hong Kong) na tailoring alishafutilia mbali kabisa. Ma house girl hawa walikuwa kama mama kwa watoto wangu, hata nikisafiri nje kwa muda mrefu hakuna lililokuwa linaharibika, wanafuatilia watoto shule japo wao walikuwa ni darasa la saba, mtoto akikosa anakaripiwa kama vile ni wake kabisa. Watoto waliwazoea kuliko wazazi. Mpaka leo wanawaita Aunt. Sina watoto wadogo tena, lakini nasema housegirls ni matatizo mnoo na sitegemei kumsaidia yeyote yule tena zaidi ya kumlipa haki yake ya mshahara. Poleni wenye familia changa.