Kwa nini mfanyabiashara yeyote anayeanza kujitafuta anatakiwa kusajili jina la biashara?

youngkato

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
3,811
Reaction score
3,888
Kwa nini mfanyabiashara yeyote anayeanza kujitafuta anatakiwa kusajili jina la biashara?



Kuna biashara nyingi mitaani zinafanya vizuri – zina wateja, zina jina zuri lakini hazijasajiliwa.

Watu wanadhani kusajili jina ni kwa matajiri au makampuni makubwa.

Hii siyo kweli.

πŸ‘‡1

Kusajili jina la biashara ni hatua ya kwanza kuelekea ukuaji wa kweli wa biashara.

Unafanya biashara yako kutambulika na watu, unapata ulinzi kisheria, na unafungulia fursa nyingi zaidi.

πŸ‘‡2

Unapata cheti rasmi kutoka BRELA kinachothibitisha kuwa wewe ndiye mmiliki halali wa jina hilo.

Hakuna mwingine ataruhusiwa kutumia jina hilo kisheria.

πŸ‘‡3

Unaweza kufungua akaunti ya benki kwa jina la biashara yako.

Hii inaongeza uaminifu kwa wateja, inakusaidia kutenganisha fedha binafsi na za biashara.

πŸ‘‡4

Unaweza kutengeneza "LIPA NAMBA" kwa jina la biashara.

Wateja wanalipa kwa jina la biashara yako badala ya jina la mtu binafsi – biashara yako inaonekana serious na ya kitaalamu.

πŸ‘‡5

Unaweza kuomba mikopo ya biashara, kuomba tenda, au hata kuomba misaada kwa mashirika.

Masharti ya kwanza huwa: β€œTuletee cheti cha usajili.”

πŸ‘‡6

Unaandaa biashara yako kuwa kampuni kubwa siku zijazo.

Majina mengi makubwa unayoona leo kama β€œAzam”, β€œVunja bei”, β€œJambo” yote yalianza kama majina ya biashara yaliyosajiliwa.

πŸ‘‡7

Siku zote sajili jina kabla hujawa mkubwa.

Jina au (brand name) linaweza kuwa na thamani kubwa kuliko bidhaa unazouza.

Usiruhusu mtu aje alisajili halafu akutake uliache.

πŸ‘‡8

Watu wengi wanatumia jina kama Fety beauty, lakini ni mmoja tu aliyelisajili.

Ukilitumia bila kujua, unaweza kuishtakiwa au kuamriwa kuliacha.

πŸ‘‡9

Mambo unayohitaji ili kusajili jina la biashara:

Kitambulisho cha Taifa (NIDA)

Jina unalotaka kutumia

Namba ya simu (yako binafsi)

Email

Anwani ya makazi na ya biashara

πŸ‘‡10

Biashara yako ni kama mtoto (Kuna siku itakuwa kubwa)

Inahitaji jina la kuzaliwa, cheti cha kuzaliwa, na utambulisho.

Jisajili. Linda jina lako. Kuwa rasmi.

πŸ‘‡11

Kupata msaada wa haraka wa kusajili jina lako, tupo tayari kukusaidia hatua kwa hatua hadi kupata cheti chako.

DM au wasiliana nasi:

πŸ“ž +255 693 880 325 wa.me/+255693880325

πŸ“ Victoria Agency Company

Mwanza - Mkolani

Minimize image
Edit image
Delete image
 
Je unapokuwa umesajili jina la biashara na kupewa cheti kuna malipo yoyote kwa kila mwaka?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…