Umaskini na ujinga wa watanzania ndiyo mtaji mkubwa wa CCM. Si kwamba wanapenda kuikumbatia CCM bali ni kutokana na kupata chochote kutoka CCM hasa chumvi, khanga, kofia na tshirt. Mtu maskini na asiye na elimu katu hawezi kuwafagilia wale wanaokuja mikono mitupu. Maana shida yake ni kumaliza matatizo yanayomkabili kwa wakati huo na si matatizo ya kesho. Kwa hiyo kwenda na sera nzuri kwa mtu maskini anaona hazimsaidii kwa kuwa yeye ana njaa leo na anahitaji kula leo. Na hapo ndipo ambapo CCM huwa inafanikiwa kwa kuwa wanatoa hizo elfu mbilimbili, na mabango ya CCM, basi wananchi wa huko maskini wanaona hawa ndiyo wenyewe.