Elections 2010 kwa nini nafurahi kikwete kuanguka jukwaani?


Usiamini kila unachosoma,

Angalia dakika ya 1:39 mpaka 1:49

"Wanachama, wapenzi, washabiki, wakereketwa na wananchi kwa ujumla" Muandishi wa wapi asiye hata na tape recorder huyu ? Au anataka kutoa mambo yaliyo untruthfully partisan ?

 
Last edited by a moderator:
Kiranga;
Una-argue na mtu ambaye hamko kwenye uelewa unaoshahibiana, na ninadhani hata elimu yenu itakuwa tofauti sana, nadhani mithili ya mtoto wa darasa la pili na profesa wa chuo kikuu. Hii ndiyo tofauti yenu na dniyo maana hamuwezi kuelewana,... utapoteza mda wako!
 
Kuna uwezekano mkubwa wewe ukawa ni Professor Juma Kapuya au yule ant Muddy almaaruf pale Kariakoo. Usiniulize ni kwanini!
 
Adui mwombee njaa atanyosha mikono hata kama alikuwa shujaa.
 
Anatakiwa aanguke uraisi, sipendi aanguke majukwaani. Mungu ampe afya njema...
 
umekosa utu; sababu zilizofanya aanguke siyo hizo 4 ulizoelezea, ni afya yake kama binadamu na hata mpinzani wake kisiasa WS amempa pole.
 
Mimi ni CCM , ingawa natofautiana na JK na CCM katika mambo kadhaa ya kimsingi lakini hili la kushangilia kuanguka Mkuu wa Nchi hadharani ni ukosefu wa ustaarabu.
Siasa si uadui, na sote ni watanzania na nafikiri ni ukosefu wa hekima kwa hali ya juu kushangilia ugonjwa wa mtu yeyote yule.
Waswahili walisema Mungu si Athumani, kile uchekeavyo kimpatapo yule uneyemfikiria adui yako , Mungu in all fairness anaweza kukupatia kama si wewe basi jamaa wa karibu sana na wewe.
Kwa hili nampa pole JK na Mola amrudishie afya yake.
 
Watu wengi na hasa viongozi wa CCM na serikali wanaliona tatizo la kuanguka kwa rais (Amiri Jeshi Mkuu) kama kitu cha kawaida tu. Mawazo yao yote yako kwenye kampeni ili waweze kuchuma pesa. Hii ni hatari kubwa kwa kiongozi wa nchi kuanguka mara kwa mara ninashauri uchunguzi wa afya yake ufanyike na kupata matibabu yanayostahili ili kumuweka katika hali nzuri ya afya yake na hali hii isitokee tena. Pia madaktari wake wawajibishwe kutokana na uzembe wa kutokuweza kutambua vizuri afya ya rais hadi anaanguka kwa mara nyingine tena!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…