Kwa nini naiheshimu baby walker yangu

Boeing 747

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2018
Posts
3,515
Reaction score
9,415
Ndugu zangu...
Picha nilizotupia zinajieleza..

Ukitafakari adha ya usafiri wa jumla mfano mwendo kasi, basi huna budi kuheshimu chombo cha usafiri ambacho mwenyenzi Mungu amekujalia kuwa nacho.

Imezoeleka sana watu wanaomiliki SUV na magari mengine makubwa kuwanyanyapaa wamiliki wa magari madogo mfano passo,vitz, ist, March to mention the few.

Ukitafakari kero za usafiri wa jumuiya, basi utagundua kuwa gari unalomiliki ni la thamani kubwa kwa sababu gari hilo linaweza kukusaidia kuondokana na adha zifuatazo.

1. Kuchelewa kazini/kwenye biashara yako

2. Kuepuka kero ya kubanana ukizingatia joto la Dar kwa Arusha msimu wa baridi ni kero kubwa unakuta watu wamejifungia vioo vyote ndani ya daladala..ukipanda tu unahisi kuishiwa pumzi...vioo vyote vinakuwa na ukungu...kama unaugua pumu hapa utakiona cha moto.

3. Kero ya kushikwa kiuno na mwanaume mwenzako

4. Kero ya kujikuta umelaza kichwa chako kwenye matiti ya mke wa mtu

5. Kero ya kuchanganywa na mifugo ndani ya daladala...hii ipo sana Arusha huko Ngaramtoni na Kikatiti, usishangae kupanda daladala na kondoo wanne mpaka sita.

6. Matusi. wahudumu wengi wa daladala wana lugha chafu sana za kukukera na kukuharibia siku.

7. Kijana mdogo wa kiume kujikuta umemshika mama mtu mzima kiuno ili usidondoke. Adha gani hii?

8. Msimu wa joto unaweza kubanana na jamaa ananuka jasho,kikwapa na wakina dada baadhi wananuka mawigi kama gari la kubeba ngozi....kuwaambia huwezi coz huwalipii nauli wewe

9. Kuibiwa ni swala la kawaida sana kuibiwa simu au wallet wakati unagombania siti

10. Wadada wenye shepu zao unabanana nao unakuta wamekugeuzia makalio basi huwa ni tafrani tupu kwa vijana rijali

11. Na kero nyingone nyiiingi ambazo sijaziweka hapa

Hitimisho.
Wewe mmiliki wa baby walker usijihisi mnyonge kisa jamaa anaendesha prado. Wote mpo ndani ya gari, wote hamnyeshewi, wote hamuungui na jua, wote mnakula kiyoyozi, wote mnauziwa peteol bei moja
na mwisho kabisa tusidharau chombo cha mtu, hakuna chombo cha moto kinachouzwa laki mbili.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahah datsun oyeeee,nazingua bana mkuu.


Yote uliyoyasema hapo juu nayaunga mkono kwa 100% mkuu.

Hio picha ya mwisho hapo mpk chalii ameota vigimbi sababu ya kusimamia ukucha kwny mwendokasi hahah.

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23][emoji23]nameandika uzi maalumu kuitetea..na mimi nivimbe mjini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji23][emoji23]Kwa kweli vijana tupambane tu tumiliki hata Boda boda....ina heshima yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…