NullPointer
JF-Expert Member
- Feb 7, 2011
- 3,461
- 2,273
Kwa nini napingana na system ya Tanzania ya NECTA, mtihani moja nchi nzima ku-determine future ya mwanafunzi ni ujinga, Mfano mzuri Mtu anayetaka kuingia vyuo vya nchi za nje anaruhusiwa kufanya SAT na ACT au TOEFL na akifeli SAT ya kwanza anauwezo wa kusoma na kujipanga baada ya miezi kama mitano anapiga SAT nyingine, ile SAT aliyopata marks za juu ndiyo anayotumia kufanya application alafu anachomoka vizuri tu na chuo anaingia, sasa hii ya mtihani moja tu wa NECTA kila umalizapo kidato cha sita, je kama mtu aliugua siku hiyo? Au mtu kakaa laboratory anafanya mtihani equipments zikagoma, manake huo mtihani anafeli kwa kosa ambalo unakuta sio la kwake, Wangeweka mitihani standard ambayo ina system kama ya SAT au ACT au TOEFL kua mwanafunzi anaweza akachukua muda wowote akijisikia yupo tayari for as long as kamaliza miaka miwili ya elimu ya advanced basi akifeli ya kwanza anauwezo wa kusoma sana kwa kipindi kama cha miezi mitatu hadi mitano kujiandaa kwa mtihani unaofuata, akifeli na huo anajaribu unaofuata, for as long as ipo siku ataweza then tatizo liko wapi, si kaweza? Mtu anayerisit na bado akaanguka haina faida yoyote wakati kapoteza mwaka, na bado akarudia tena akasosa, ukizingatia mitihani ya private candidates ilivyo ya ovyo inafika kipindi mtu kapoteza miaka minne bure, Huu mtihani wa NECTA kuna vijana walikua vizuri sana kichwani ambao hata shuleni hawakuwahi kupata chini ya 1.5 lakini hii NECTA ilichowafanyia, nchi nzima hakuna A wala B ya Physics ina maana nchi nzima ina wajinga ambao hawawezi Physics? Si kweli, na kama system ninayoongelea ingekuwepo basi mtu angeweka ku-register na baada ya miezi kama mitano akafanya mtihani tena, kama ni yote mitatu au moja anaotaka kuongeza marks mfano ana div III ya point 7 kwa sababu ya F ya GS, mtu kama huyu si mjinga kiasi kwamba akashindwa kusoma GS miezi miwili na akaweza kufikisha S, angeweza rudia GS peke yake na kurekebisha marks then ndiyo cheti kikatolewa.. Tusijitahidi kuwakosesha wanafunzi wa Tanzania nafasi za kuingia vyuo vikuu bali tujitahidi kuwapa nafasi za wao kuingia, kuwapa moyo wa kusoma kwa bidii ili wafaulu, moyo wa wao kutaka kua na marks za juu,Nikiona Tanzania, competition inabaki kwenye shule zisizozidi 5, hizo nyingine wanafunzi hawana muda na competition vijana wameharibikiwa moja kwa moja. Is this a nation that we are building au ndiyo tunaliharibu!!!
Mi nimemaliza mwaka huu PCM, mtihani naukumbuka vizuri ulivyokua ingawa sijafeli ndiyo lakini still nikikumbuka mfano Physics Practical Paper 2, hakuna aliyetoka anafurahia ule mtihani, si kua ulikua mgumu hapana, bali unaufanya unatoka hujui ulichokifanya ni nini kisa data zilizopatikana na experiments walioleta ni za ajabu ajabu tu, Sometimes tusijaribu kuleta kitu kipya kwa wanafunzi ambacho kitampotezea saa nzima kufikiri kupata jibu huku unajua strict kabisa kuna shule laboratory wanaingia mara tano tu miaka yote miwil.