meningitis
JF-Expert Member
- Nov 17, 2010
- 8,425
- 4,768
wakuu mgomo wa madaktari unaendelea kushika kasi,ni mgomo unaweka historia kwa kuhusisha sehemu kubwa ya tanzania.ninavyoona wizara ya afya imeshindwa kutatua mgogoro huu kwani wao ndio sehemu ya tatizo kwa hiyo ni wazi waziri mkuu anahusika kutatua mgogoro huu kwa sasa.jana ilionekana kama PM ataenda kuwasikiliza madaktari na kujaribu kutatua mgogoro huu.lakini hajafanya hivyo na badala anamtuma waziri wa afya kuongea na waandishi wa habari.tafsiri yangu ni kuwa bado serikali inaendeleza dharau kwa madaktari,bado serikali haijaona madhara ya mgomo huu.kwa nini PM hafanyi uamuzi sahihi wa kukutana na kuwasikiliza madaktari?je anasubiri vifo zaidi vya wapiga kura au anaona ni utani?au anasubiri wananchi waingie mabarabarani?
Pinda kutana na madaktari!! Usisubiri maamuzi magumu ya wananchi.
Pinda kutana na madaktari!! Usisubiri maamuzi magumu ya wananchi.