Kwa Nini RADI haipigi mijini?

GAMBLER

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2009
Posts
303
Reaction score
11
Mara nyingi nimekuwa nikisikia katika vyombo vya habari kuwa watu wamepigwa na radi wakiwa shambani au wako baharini wakivua, sijawahi kusikia radi imepiga mjini, Kuna sababu yoyote inayofanya radi isipige mijini? Ninaomba wajuvi watupe darasa kidogo
 
Radi nyingi ni za kutengenezwa kiuchawi.
Wachawi wengi wanaishi nje ya miji,
thats y mijini hazionekani.
 
Sina uhakika wa kisayansi ila nadhani mazingira ya vijijini yanachangia kwa kiasi kikubwa kuliko mazingira ya mijini.Vijijini mara nyingi mazingira yake yametawaliwa na misitu mikubwa ambayo uvutia zaidi radi kupiga sehemu hizo.
 
sina uhakika wa kisayansi ila nadhani mazingira ya vijijini yanachangia kwa kiasi kikubwa kuliko mazingira ya mijini.vijijini mara nyingi mazingira yake yametawaliwa na misitu mikubwa ambayo uvutia zaidi radi kupiga sehemu hizo.

vipi dodoma ambako misitu ni nadharia ya kufikirika?
 
mm nahisi pengine kwa vile mijini hakuna miti mingi ukitaka kuamini chunguza wengi hupigwa na radi wakiwa chini ya miti huko mashambani wakiandaa hayo mashamba,NI MTAZAMO TU
 
vipi dodoma ambako misitu ni nadharia ya kufikirika?

Mkuu buji naomba ufafanuzi kidogo wa hili swala.
Niliipata moja kuna mheshimiwa fulani alikua anaenda kukagua maendeleo yakilimo sehemu fulani, wakati anaenda mashamba ya pamba yalikua kwishen, yaani hmna kitu. Kesho yake wakati anarudi jijini Dar alishangwaza na jinsi pamba livyokua umestawi katika mashamba yale yale aliyopita siku moja kabla na yalikua kame.
Na kuna Theory nyingine mheshimiwa nanihii alininginiza koti hewani akiwa anpiga mkutano ili kuonyesha wazee wa eneo hilo kua yeye ni mkali katika yale Mambo.

Binafsi mimi sio muumini wa hizi sayansi ningependa kama kuna m2 yeyote aliye na ushuhuda kamili wa haya mambo atujuze.

Juzi tu TV yangu imepigwa radi hapa Iringa. sasa sijui ndio hizo za kutengeneza coz jinsi ilivyopigwa ilibidi nicheke
Hivi kuna uwezekano mtu akatengeneza radi?
 
Nijuavyo mi radi ni electrical charges ambazo mara zizalishwapo huko mawinguni hutafuta mahala pakupita. Na kitu chochote kilicho kirefu kuliko vingine kina hatar ya kupitiwa na hizi charges kuelekea ardhini. Ni kama utakaposhika waya wenye umeme ulio-uchi wakat uko peku charges za umeme zitaenda ardhini kupitia mwili wako.

Hivyo in short vitu virefu ktk eneo husika viko hatarin zaidi radi itakapopiga. Ndo maana majengo marefu yana waya kutoka juu ya jengo mpaka ardhini kuruhusu charges za radi zipite huko. Kumbuka waya huo unakua mrefu zaidi ya jengo ili ndio uwe wa kwanza kukusanya charges za radi.

Vijijini hasa sehemu za tambarare miti hakuna au vichaka tu binadamu anakua yeye ndio mrefu kuliko kitu kingine ktk eneo husika la radi. Hivyo charges za radi zanakutana na kichwa cha binadamu, zinatumia mwili wake kwenda ardhini. KIFO!

Kama kuna miti mirefu sio ishu kwa sababu mti mrefu kuliko yote ndo itachanwa kwa radi. Na kama uko chini ya huo mti umeushika, wewe na huo mti mtaaga dunia au kujeruhiwa vibaya!

Mi kwa uelewa wangu mdogo nikiona niko eneo tambarare hakuna miti na radi inatandika ntalala chini angalau inaweza kuniokoa. Huenda kuna vitu vingine virefu vitatandikwa na charges za radi.

Asante.
 
umedadavua inavyopaswa mkuu, mtoa mada chukua jibu lako
 
mkuu una tahadhari sana,ulale chini kwenye mbuga?.
 
mm nahisi pengine kwa vile mijini hakuna miti mingi ukitaka kuamini chunguza wengi hupigwa na radi wakiwa chini ya miti huko mashambani wakiandaa hayo mashamba,NI MTAZAMO TU

Uko sahihi mkuu! Mara nyingi radi utangulia kupiga vile vitu vilivyo virefu angani kama: miti mirefu, communication towels nk. Minara ya mawasiliano uzuri ufungwa solid earthing hivyo kupunguza effect ya lightning stroke, lakini bado kama magnituge ya radi ni kubwa, minara nayo uathirika.
 
Radi ni mkondo unaosafiri kutoka mawinguni kuelekea ardhini. huwa unatafuta kitu kirefu zaidi ili ikifanye njia. unashauriwa usitembee sehemu ya tambalale kama wewe unaona ndo kitu kirefu zaidi wakati wa uwezekano wa kutokea radi. Pia usikae chini ya vitu virefu zaidi kama miti. Utafiti unaonesha mtu anayekimbia hupunguza uwezekano wa kupigwa na radi kwakuwa muda mwingi hagusi chini.
Kuepika kari majumbani ni muhimu kuweka waya wa earth unaochomoza juu na kwenda chini kama nyumbayako ipo pekeyake pekeyake na ni ndefu kidogo.
Kwa mpangilio wa nyumba za vijijini (umbali mkubwa kutoka nyumba hadi nyumba) si ajabu kusikia watu wamepigwa radi. Vivyo hivyo kwa wavuvi baharini
 
Jibu ndio hilo la Tripo9 majengo yote na minara ya simu huwekewa vifaa maalumu kwa ajili ya kuzuia Radi (Thunderstorm)



 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…