Kwa nini Raia Wanachukua sheria Mikononi?

Idimi

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2007
Posts
15,328
Reaction score
11,192






Ndugu wana JF, hii tabia ya wananchi kujichukulia sheria mmikononi imekuwa sugu sasa. Suala la watuhumiwa vibaka kuuawa, watu kuvamia vituo vya polisi nk limekuwa tata sana. Shida iko wapi lakini? Kuna tatizo gani hapa? Utatuzi wa suala hili ni upi? Tufanye nini?
 
SABABU ZA RAIA KUCHUKUA SHERIA MKONONI NI KUTOKANA NA UDHAIFU WA ...sheria yenyewe,wananchi,wasimamizi ya sheria(POLISI,MAHAKAMA)na jamii kwa ujumla wake....!
CHUKUA MFANO WA KIBAKA/JAMBAZI(mhalifu yeyote) ANAPOKAMATWA AU KUPELEKWA KITUO CHA POLISI/MAHAKAMANI......IT HADLY TAKE FEW DAYS.....UTAMUONA MTU HUYU MTAANI TENA AKIRUDI KWA KASI MPYA KABISA.....HII INAWAFANYA WANANCHI WAONE HAKUNA MAANA KUWAPELEKA WAHALIFU WAO polisi/mahakamani KWANI WATARUDI KUTENDA TENA UHALIFU.......! WAKATI WANANCHI WANATAKA KUISHI KWA AMANI NA STAREHE NA KULALA MILANGO WAZI (kumbuka kipindi cha mzee wa nji hii alipokuwa interior minister).....! WAKIONA MALENGO YAO HAYATIMII KILICHOPO NI KUWATOWESHA TU WAHALIFU.......!
 
nafikiri mmesahau lile tukio la Zombe kuwaamuru wezi wake wawamiminie risasi wale wafanyabiashara wa madini kwa kisingizio kuwa ni majambazi na kisha wakapora yale mamilioni yao haya ni mojawapo ya mambo yanayofanya raia wanajichukulia sheria
 
Raia wa Tanzania wanachukua sheria mikononi kwa sababu Viongozi hawafuati sheria,wanapindisha sheria,hawaheshimu utu wa wanaowaongoza,wametanguliza pesa mbele.Mahakam na Polisi hazitendi haki,wanaofungwa ni wasio na uwezo(dagaa)kina papa wakifanya makosa wanadhurura mitaani bila wasiwasi (kumbukeni Ukiwaona D.M).Je, mwajua wahindi na waarabu ndiyo wanyanyasaji wakubwa? je,mmeshawahi kuwakuta jela? hayo ndiyo yanayowafanya watu wachukue sheria mikononi,kwa ufupi sababu kubwa ni utawala mbovu kuanzia chini mpaka Taifa, wazungu wanaita 'bad governance'
 
Suala la raia kuchukua sheria mkononi kwangu mimi naona ni sawa tu,nasema hivyo kwa sababu inatokea mnamkamata muhalifu halafu kweli mnamfikisha mahakamani kwa ushahidi wa kutosha lakini baada ya siku mbili mnakutana na mtuhumiwa barabarani tena sio kwa dhamana bali kuachiliwa kabisa.Kama sio police kunamasiala ni nini.

Lakini wakubwa wetu tunawambia kila siku kwamba uvumilivu unamwisho hili naomba likae akilini mwenu,tumechoka na serikali iliyojaa ukilitimba,sasa ni bora sisi wenyewe tuwe mahakimu na tunamalizana badala ya kuanza kusumbuana na police.
 

Lakini kuchukua sheria za mikononi kusiishie kwa vibaka na wakosaji wadogo wadogo....vipi mafisadi ambao tunawajua wazi, wezi wa pesa zetu EPA nawao tuwachulie hatukua mikononi situnajua majina yao na mali zao? hata wanapoishi?
 
Lakini kuchukua sheria za mikononi kusiishie kwa vibaka na wakosaji wadogo wadogo....vipi mafisadi ambao tunawajua wazi, wezi wa pesa zetu EPA nawao tuwachulie hatukua mikononi situnajua majina yao na mali zao? hata wanapoishi?
UKICHUKUA SHERIA MKONONI KWA MAFISADI WAKUBWA........WANATETEWA......! cheki tulivyojigaia shamba la fisadi walivyokuja kulindana......!
 
UKICHUKUA SHERIA MKONONI KWA MAFISADI WAKUBWA........WANATETEWA......! cheki tulivyojigaia shamba la fisadi walivyokuja kulindana......!

Na mwisho wa yote itakuwa nini basi?
Kama leo watu wanajigawia mashamba ya mafisadi, kesho wataigawia migodi, magari na viwanda,......then?
Patakalika?
 
Na mwisho wa yote itakuwa nini basi?
Kama leo watu wanajigawia mashamba ya mafisadi, kesho wataigawia migodi, magari na viwanda,......then?
Patakalika?
ITABIDI PAKALIKE TU.....! HAPO CHUKULIA MTU ALIYEJINEEMESHA KWA KUKWIBA VYA WATU, WENYEWE(WALIOIBIWA) WANAMUONA NA KUVIONA VITU VYAO....NI NONSENSE KUVIEKA VILE VITU KUENDELEA KUKAA POLISI AU MAHAKAMANI KAMA VDHIBITI.....VIRUDISHWE KWA WENYEWE WATU WAENDELEE NA SHUGHULI ZAO........DELAYING ZA MAHAKAMANI HUSABABISHA PIA WATU KUFANYA JUSTICE WAO WENYEWE(sio kuchukua sheria mkononi)KWANI PROFFESSIONAL JUSTICE MAKERS WAMEFISADIKA.....!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…