Kwa nini simu ya mume iogopwe kama ukoma?


BAK,

Nadhani tunahitaji kuelewana kwanza kwenye hoja ya msingi. Sijasema popote kuwa, mtu akiwa huru na simu ya mwenzi wake ni sawa na kuipekua pekua. Pia simaanishi kwa lolote kuwa usipokuta call au sms za wapenzi wa mwenzi wako ina maana kuwa huyo ha-cheat. No, don't miss the point.

Swali langu la msingi ni kuwa, kama wewe na mwenzi wako mnashiriki kila kitu, unaanzia wapi kudai kuwa simu ni personal kwa hiyo hana ruhusa ya kuishika? Hapa tunaongelea suala la kuweka mipaka ya kugusa na hata kutumia simu ya mkeo/mumeo na vitu vingine kama email, bank cards etc.
 
.....Kikubwa hapa ni kuaminiana, lakini mhhhh hata mimi nina tabia ya kupekua simu ya Mr.


Poa ndugu yangu. Huwezi kumuamini mtu ambaye anakuwekea vikwazo na vitu vyake. Mbona kwenye 6x6 kila kitu ni kiko kwenye "trade free zone" halafu akitoka hapo aanze kukuambia kuwa, ahhh simu yangu usiiguse, ohhh kadi yangu ya bank ni private affair!! Mimi silewi kabisa. Ila kupekua pekua siyo vizuri na especially kama una ruhusa ya kuigusa bila kusababisha kipingo cha mbwa mwizi, tena yule mbwa koko!!
 

........Nipo huru kugusa simu yake muda wowote na yeye vile vile yupo huru.
Hao watu wenye private kwenye simu zao kuna kitu wanaficha.Kama mmekuwa mwili mmoja ya nini kumkatalia mwenzio kugusa simu yako?

Hata hizo kadi za bank inabidi mtu usiwe msiri kwa mke/mume, mpe mwenzio password hata kesho ikitokea shida mtu anaweza kwenda kuchukua pesa kwenye ATM.
 


Yaani umenigusa penyewe. Eti watu muwe mwili mmoja lakini simu no access, bank card out of bound, email password ndo usiseme. Hapo mimi nasema ni big NO. Kwani huyo mume au mke anafanya kazi za state security (na ushushu wao) ambayo iko juu ya family security??? No way, kama ni huo usiri kwa mpenzi wangu sina sababu ya kumwita mpenzi wangu, huyo labda awe ni mtumishi tu.
 

...hapana bana,

vyote ulivyotaja 'ni vyangu', na hakuna yeyote anayepaswa ku access,..kuanzia phonebook yangu, message inbox na outbox,...email address, bank account! hata mawazo yangu namueleza 75% tu ya ukweli, 25% nakaa nayo akiba.

Yeye naye sitaki wala kugusa simu yake,wala email yake wala sina haja kujiumiza kiutaka kujua ukweli wa moyoni/mawazoni mwake.
Binaadamu haaminiki bana, mwenzako nishaumwa na nyoka, Never again!
BTW, nadhani siku hizi anajua hapa Jamii forum natumia jina la MBU, sijui nibadilishe?

Kila la heri nyie mnaoaminiana.
 


Thank you Mkuu. We're on the same page when it comes to this issue. Eti unashika simu ya mkeo/mumeo na labda kuipekuapekua kuhakikisha namba zote za simu zilizopigwa na kuingia unazifahamu na txt messages zote zilizoingia na kutoka hazina athari katika ndoa yenu.

Mkuu DC, Simu kwa maoni yangu ni personal kama wewe unaona vinginevyo then you're entitled to your opinion. Pia usitake kuwalazimisha watu wafanye kile ambacho wewe na mkeo mnakifanya kwamba hamna embargo kwenye simu zenu.

Ndoa moja inatofauti kubwa sana na ndoa nyingine. Unaweza kusikia mambo yanayofanyika katika ndoa moja ukabaki mdomo wazi na mambo hayo hayo yakifanyika ndoa nyingine yanaweza kabisa kuwa ni chanzo cha kuvunjika ndoa. Kwa mfamo kuna wanandoa wengine wana bank account moja na kila mmoja anajua nini kinachoingia toka kwa mwenzake, wengine kila mtu ana bank account yake na wana bank account tofauti ambayo hii ni kwa ajili ya daily expenses zao na wote hawana access za personal bank account za mwenzao.


Binadamu ni mwerevu sana kuliko mnavyodhani. Mwanandoa anaweza kabisa kuamua kumuheshimu mkewe/mumewe na hivyo kutokuwa na extra activities outside their marriage, lakini akiamua kufanya otherwise anaweza kabisa kufanya hivyo na wala mwenzie asigundue hata kwa miaka chungu nzima.

Kuna njia nyingi sana ambazo binadamu anaweza kutumia ili kufanikisha hizo extra activities nje ya ndoa simu ya mkono ni mojawapo lakini kuna nyingi nyinginezo. Hata kabla simu za mkono hazijaingia duniani/Tanzania wake kwa waume walikuwa wanatoka nje ya ndoa zao.

Kwa hiyo hilo hitimisho lako kwamba wanandoa wanaoweka vikwazo katika simu zao hawajiamini kwenye suala la uaminifu katika ndoa si sahihi hata kidogo. Kama wewe na mkeo hamna privacy basi hilo ni zuri sana kwenye ndoa yenu lakini si kithibitisho kwamba kwa kuwa hamna privacy basi mmoja wenu hawezi kuwa anacheza viwanja vya ugenini.

Nimekupa mfano wa jamaa aliyeamua kutembea na simu ya mkewe kwa masaa chungu nzima na hakugundua kitu, lakini alipoomba passwords za e_addresses za mkewe alikataa kata kata. Na yanayofanyika ndani ya ndoa yako usitake kuyafanya yawe kigezo cha ndoa nyingine chungu nzima. Kwenye ndoa nyingine wanandoa wanaona simu ni personal item hivyo wamejiwekea mipaka hiyo ambayo wote wanaiheshimu.
 
Taarifa ndani ya simu ni mali binafsi, hii ina maana hata kama husband/wife ndo kanunua simu, haruhusiwi kupekua yaliyomo. Huu ndio tunaita uhuru binafsi. Tatizo hapa si kucheat wala nini. Tatizo kuna sms nyingine zinaweza zikatafsirika vinginevyo. Mmekuwa mwili mmoja, what a hell is this?
 

Mwalimu Z,

Nimesema mara nyingi kwamba simaanishi kuwa mtu apekue pekue simu au email ya mwenzake kila wakati. Ninachotatizwa nacho ni kuwekeana vikwazo kiasi kwamba mtu akigusa tu, anapata corporal punishment kama huyo dada alieyepigwa hadi kupata miscarriage. Kwani kuna nini kinafichwa?

Mimi nampa heshima my wife kwa hiyo siwezi kupekua pekua simu au pochi yake. Hata hivyo, ninu uhuru wa kuigusa na kufanya lolote. Hata akinikuta napekua kwa sababu yoyote hawezi kujinyonga! Naye nikimkuta anapekua nacheka tu, mara nyingi anatumia msemo wa utani kuwa, "kila abiria achunge mzigo wake". We are happy.

Lakini alivyosema BAK, hatuna maana kuwa kila mtu aishi kama sisi. Ndo maana tunafurahi kupata maoni na uzoefu wa wengine. Diversity is the real meaning of life. I am sure nobody is being offended!
 
hii sredi inawagusa wengi kweli kweli!.....

nimeona ugomvi mkubwa kweli jana usiku huku kigoma KUHUSIANA NA SIMU YA MKONONI

ninashauri ''iendelee kuwa personal''
 
hii sredi inawagusa wengi kweli kweli!.....

nimeona ugomvi mkubwa kweli jana usiku huku kigoma KUHUSIANA NA SIMU YA MKONONI

ninashauri ''iendelee kuwa personal''

Sawa G,

Bila vikwazo na maguvu kama ya jeshi lakini?
 


Twandefiki,
Physically sikufahamu, lakini nimefuatilia arguments zako (maandishi yana sauti) naiona sura yako mbele yangu na jinsi ulivyo na jazba katika ku-argue juu ya mada hii. Si pingi wala sikuungi sana mkono kuhusu hoja zako, kwangu mimi naziona zipo 50 kwa 50.

Kingine kinachoonekana kati yenu wewe na DarkCity, ni uzoefu mdogo sana katika mambo ya ndoa (tafadhali nikosoe), yawezekana ndoa yenu ina umri usiozidi miaka 5, hali ambayo inawanyima kuona madhara ya kufuatilia kila kitu mwenza wako anachokifanya. Kweli kwenye ndoa lazima kuwe na transparency, lakini jua mtu na mume/mke wake ni nafsi 2 tofauti. Nafsi 2 kamwe haziwezi kuwa sawa, kila nafsi ina namna ya ku-interact na the outside world, how or in what ways it depends. Ninachokijua mimi, jiamini wewe mwenyewe, ukijiamini huna haja ya kufuata cm ya mwenza wako, ukiifuata maana yake ni kwamba wewe mwenyewe hujiamini (unajua namna ambavyo umewahi kum-cheat na ndio maana unapekua pekua cm yake).

Nimependa maoni ya wote waliochangia. Hatuwezi wote kuliona katika hali ya usawa jambo kama hili kwani tunatofauti katika uzoefu na mambo ya ndoa, tamaduni na desturi nazo tunatofautiana, elimu tunatofautiana, na nafsi (self) tuatofautiana, otherwise is a good and hot mada. For me I regard all arguments are valid.
 


Fugwe,

Nimekumiminia siyo senksi tu bali nimekupashia pia!!

Hatuwezi wote kufanana. Kwa hiyo ni jambo la muhimu sana kwa binadamu mwenye hekima kuwasikiliza wenzake na kuwaheshimu pia hata kama mnatofautiana kwa kiasi kikubwa sana. Waafrika kwa kiwango kikubwa tumekuwa na uvumilivu mdogo kwa watu wenye hoja tofauti na zao. Mimi nawaheshimu wote waliotoa maoni yao hata kama tumetofautiana na hasa hasa pale ambapo hawajaribu kumshambulia aliyetoa maoni kabla yao. Kama ni suala la uzoefu nadhani lisikupe tatizo. Jaribu kuchukungulia posts za nyuma kidogo, nimeshatoa ufafanuzi. Tuendelee kujadili na kumegeana hiki chakula cha fikra!
 


Tuseme mmekuwa pamoja kwa muda wa miaka 20 (9+11), kama muweza ku-maintain kwa muda wote huo ni vizuri. Mmejiwekea kanuni yenu ya kila mmoja ku-access simu ya mwenzake, hiyo ni kanuni yenu. Mimi ndoa yangu ina umri wa miaka 20, hatukuweka kanuni ya kushika au kutoshika cm ya mwingine bali kwa vile watu wazima tunajua ukimchunguza sana kuku hautamula na ndio maana tumefika hapo tulipo. Kweli kila ndoa na kanuni zake la muhimu ziwaletee raha na amani kwenye ndoa yenu. Kama ni hivyo basi usiyumbishwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…