Kwa nini sina imani na wabunge wa CCM katika suala la katiba

Kwa nini sina imani na wabunge wa CCM katika suala la katiba

crome20

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2010
Posts
1,193
Reaction score
810
Baada ya mapambano ya muda mrefu kuhusu kuandikwa kwa katiba mpya, sasa Tanzania imeanza kuandika historia mpya kwa kuandika katiba itakayoshirikisha wananchi wote. Lakini pamoja na furaha niliyonayo, ninapata wasiwasi na wajumbe wa Bunge la katiba kutoka CCM. Kwa nini? Kwa sababu zifuatazo ambazo nadiriki kusema wamekuwa hawangalii maslahi ya Taifa zaidi ya kufikiria kupambana na upinzani hata kwa manbo yaliyo wazi. Ebu kumbukeni yafuatayo:

1
. Katiba mpya sio sera ya CCM, hivyo tokea mwanzo hwakuwahi kuona mapungufu makubwa ya katiba yetu na walidiriki hata kupinga kwa nguvu zote kuandika katiba mpya ili mambo kama ya tume huru ya uchaguzi yasipate nafasi.

2. Ni hawahawa CCM waliopinga kwa nguvu zote suala la mgombea binafsi ili kumkomoa Mch Mtikila. Lakini hata baada ya Mtikila kuwabwaga mahakamani, walitumia wingi wao bungeni kubadili katiba na kuingiza kipengele cha kuzuia mtu asigombee mpaka apitie kwenye Chama cha siasa. Hata baada ya Mwl Nyerere kulitolea ufafanuzi kwa mifano ya akina Sarwat aliyesimama kama mgombea binafsi na kuishinda Tanu, bado kile kibwagizo cha kumuenzi Baba wa taifa kilikufa ilimradi Mtikila asigombee. Sasa hivi baada ya kubanwa wanasema mgombea binafsi haepukiki lo! maajabu haya.

3:Ni CCM hawahawa waliopitisha kwa mbwembe sheria ya kutoa rushwa kwa jina la TAKRIMA ili kuhalalisha rushwa kwenye uchaguzi na kama si wana harakati kupambana tulikuwa tumekwisha. Ajabu hata wasomi ndani ya CCM walikuwa kama chekechea tu wasioweza kutumia hata 1/10 ya ufahamu wao kuliokoa Taifa na kansa ya Rushwa. Kwa ujumla mambo ya maslahi ya kitaifa yanapoletwa na upinzani akili zao zinahama wanakimbilia ushabikiki wa kipuuzi tu, kumbuka suala la posho bungeni sasa Mwenyekiti wao analalamika vikao vya kulipana posho tu visivyo na tija.

4
. Ni CCM hawa waliofanya mabaraza ya Katiba yasiwe na tija baada ya kuwaandaa watu wao tena kwa waraka wapinge maoni ya wananchi ambayo yanatishia uhai wa chama chao.Ilifika nyakati Jaji Warioba alilazimika kutoa ufafanuzi kuwa acha kukariri ya CCM, sisi tunao huo waraka semeni ya kwenu. Ndio maana kuwepo Wabunge wa CCM kwenye bunge la katiba kumepunguza furaha yangu baada ya kuona katiba inaweza kuwa mvinyo ya zamani katika viriba vipya .

NAWASILISHA
 
Back
Top Bottom