Kwa nini SIPATI WANGU WA MAISHA HAPA JF.

Joined
Apr 10, 2012
Posts
33
Reaction score
2
Nahitaji mwenzi wa maisha mwenye sifa hizi. 1. Awe mwaminifu 2. Mkweli na mpole 3. Elimu Diploma ama Bachelor degree. 4. Kabila yoyote, msukuma, msambaa, mnyakyusa, muha ama mmakonde watapewa kipaumbele. 5. umbo mrefu wastani 165cm-175cm. awe miguu minene mwili wa wastani. 6. awe aidha hajazaa ama ana mtoto mmoja. 7. Dini awe mkristo na mcha Mungu 8. Umri miaka 23-27. SIFA ZANGU 1. Umri miaka 33. 2.Elimu Bachelor degree 3.Dini mkristo 4.Mrefu 180cm umbo wastani maji ya kunde. Tafakari kwa kina.
 
Duu nilidhan we ni bint!!!!!!!!

Basi muone Madam B muende chumbani muelewane kiutuuzimaaaaaas.......
 
Kwahiyo unategemea kila unapokuwa upate wakwako wa maisha? Una hatari wewe!
 
Sijaona mahali ulipotaja jinsia yako au unatafuta yeyote tu? maana hata wanawake nao hupenda wanaume wenye miguu minene au mirefu
 
Daaaah, humu ndani mnaoana kiusomi kiusomi........ Yameisha kaka!!! Basi aje huku Uru Kishumundu, nimpe shangazi yangu Dada Neema Y. Masawe

mbona unamgawa kama pipi kijiti,unamfahamu huyo vizur lakn au?
 
kulikoni kugombana wakati nahitaji tafakari ya kina ndipo uijibu hii thread. mke mwema atafanya maamuzi kwa kuzingatia falsafa yake ya maisha aliyojiwekea.
 
Huyo mkristo gani ambaye keshazaa mtoto nje ya ndoa jamani!!!! Au unatafuta mjane, kuwa muwazi
 
Ulioanza nao tangu unabalehe hadi leo wako wapi?? Tujibu hilo kwanza.
 
Kwanini hupati huko unakofanyia kazi?
 
kwani mimi na wewe tulipelekana chumbani
:dance:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…