mmmh we unaona tz na kenya hazifanani hata kwa jambo mojaYaani hivyo tu ndio vimekufanya uamini tunafanana!!
Bado hujanishawishi
Na ni watani wa jadi haswa. Mkenya anaona raha kumtania mtanzania na mtanzania anaona raha kumtania mkenya.Eti Nyang'au na Bongolala wanafanana? We acha bana! 😀
Mtu yoyote anaewaongelea watanzania kama watu wa aina moja bhasi hawajui watanzania vizuri.....Leo hii ndio mnajiuliza maswali ya msingi kama hayo, miaka ya hivi majuzi hapakua na Tanzania wala Kenya, kabla mzungu hajaja na kuchora mpaka na kuwaambia wa huko wajiite Watanzania na wa huku waitwe Wakenya. Kawakuta Wamaasai na Wajaluo, Wadigo n.k. na kuchora mpaka ndani yao hata baina ya ndugu ambao wanachangia baba na mama.
Tatizo ni kwamba Tanzania, Nyerere alianza kufanya experiments/majaribio ya mifumo ya kiujamaa kwa kuiga Warusi na Wachina halafu akaja kuyatelekezea kati na kuwachanganya kiasi kwamba mpo mpo tu, hamjijui kama nyie wajamaa au mabepari, imeshindikana kuamua kimoja sasa mnaishia kuwa na chuki na wivu kwa sisi wengine ambao tulikomaa na mfumo mmoja.
Mtanzania akitoka na kuingia Kenya au Uganda anaishia kuwa mwoga mwoga na kushangaa shangaa, akirudi kwao anaongea mabaya tu, hana lolote nzuri la kusema. Lakini Mkenya akiingia Tanzania au Uganda anajimix tena kwa muda mfupi na kuendana na yeyote bila uwoga wowote. Mimi ilinichukua muda mfupi sana kuwa mchakarikaji na mtu wa mishe ndani ya hiyo Dar yenu.
Mtu yoyote anaewaongelea watanzania kama watu wa aina moja bhasi hawajui watanzania vizuri.....
Shukuruni sana capital city yenu kuwa mainland siku zote na sio coast maana tabia za watu wa coast ilivyo dar na mombasa ni moja.. Tabia za watu wa bara napo hivyo hivyo hivyo, ukifika dar na kuweka conclusion ya Tz nzima unakosea sana na tena sana.
Kama unawajua watanzania bhasi utajua kuwa dar haijajengwa na wazaramo wala wandengereko wa pwani bali watu wa bara... unaposema watanzania waoga waoga uliwapima wa jamii zipi yaani wahaya , wachagga, wabena ,wasukuma ,wajaluo au wakurya ???..... na nimekutajia makabila ili uelewe vizuri
Mdigo wa Tanga na mdigo wa mombasa wala hawana tofauti. hao wakikuyu wajaluo, wamasai, wakurya, wakamba ni seti moja na wakurya, wajaluo,wamasai na wachagga wa Tanzania...
Ubepari umewafanya muwe aggressive kuliko watanzania lakini haimaanishi jamii zote za Kenya ni aggressive kuliko jamii zote za Tanzania.. ukija siku nyingine Tanzania fanya research yako
Kweli kabisa. Walianza kutaniana zamani sana. Sema siku hizi kuna mitandao ya kijamii enzi zile walikuwa wanarushiana vijembe kwenye semina na vikao vya maana. Washenzi sana hao wazee wa enzi hizo. 😀Na ni watani wa jadi haswa. Mkenya anaona raha kumtania mtanzania na mtanzania anaona raha kumtania mkenya.
Wapi nimeleta ligi hapo ..nimefananisha tabia za watu wa pwani ya Kenya na Tanzania na kuona ni moja ni kama nilivyofananisha watu wa bara wa Kenya na Tz..Hata wewe unafanya ule ule ujinga wenu wa kila siku kuzodoa watu wa Pwani, ustaarabu umefika Pwani kabla ya huko Mikoani, kwa maana nyingine Pwani ndiyo Tanzania, watu wa Mikoani bila ya Pwani hakuna Tanzania msisahau hilo, hata kunywa chai na kitoweo asubuhi ni ustaarabu wa Pwani, elimu yenyewe kusoma na kuandika kulianzia Pwani ndo kukasambaa Mikoani, hata jina la Tanga-Nyika hiyo ndo maana yake yaani Tanga (Pwani) na Nyika (msitu), hivyo kuwa mwangalifu kidogo kwenye haya mambo na usilete dharau na kejeli kwenye mambo ambayo nafikiri hata hauyaelewi.
Punchline!
Sitaki kuleta ligi zenu za kijinga za Pwani vs Mikoani, TZ vs Kenya bali nilitaka kuweka rekodi sawa, hizo dharau zenu hazina mshiko kwani mchango wa Mikoani kwenye TZ ni mdogo ulikinganisisha na Pwani!
Tatizo asili ya ulichoongea si sisi. Soma historia baba ujue mifumo ya kiutawala chimbuko lake wapi! Uganda, Ghana, Zambia, Zimbabwe na hata South Africa hufanya hivyo pia.Hivyo ni baadhi tu, nikiwa huko kuna wakati naona kama niko Bongo tu!