Wakuu wote tiumeshuhudia moto wa matokeo ya Kidato cha Nne 2012 ambao umehitimishwa kwa kuunda tume ya kuchunguza chanzo cha jambo ambalo sababu zake ziko wazi kabisa. Ikumbukwe kuwa matokeo ya Darasa la saba pia yalikuwa mabaya sana kiasi ambacho ilibidi Maafisa Elimu wakajichimbie tena kuchagua wanafunzi kwa lengo la kujaza madarasa. kwa nini Tume haikuundwa kuchunguza hayo matokeo hasa ukizingatia kuwa kama hakuna kiwango kizuri cha kufaulu wanapelekwa sekondari kujaza madarasa bila kujali vigezo na masharti, je hauoni kuwa kila mwaka tutakuwa na tume ya kuwachunguza hao wanaojaza madarasa wanapomaliza sekondari?
Tafakari, chukua hatua
Tafakari, chukua hatua