Juzi juzi tu hivi niliandika makala moja ndeefuuuu!!!! Iliyohusu umuhimu wa mabadiliko ya kisiasa hapa tz. Najua watu wengi iliwachosha sana na nilijua hivyo ndio maana nilianza na mkwara kidogo kwa wadogo zangu (najua wazee hawana matatizo na makala ndefu).
Leo niko na mchakato wa katiba mpya unaoendelea kwa sasa. Hii kitu ni muhimu sana wala usipime. Lakini ni vizuri pia kuwa na mawazo tofauti kidogo kwa sababu bila kuwa na mgongano wa mawazo hakuna maendeleo. Nionavyo ni kwamba watu wengi wameweka matumaini makubwa sana kwenye katiba mpya kwamba itakua mwarobaini wa matatizo, lakini ukweli ni kwamba hamna katiba nzuri kokote duniani iliyosaidia kuleta maendeleo. Katiba huwa zinajaribu kulinda maendeleo na ustawi uliopatikana. Sisemi kwamba mjadala wa katiba unaoendelea sio muhimu la hasha, ila tujaribu hata kuwaelimisha wananchi ukweli kwamba katiba imechangia sehemu tu ya matatizo tuliyonayo.
Nchi zote zilizopiga hatua kimaendeleo sababu yake ni kwamba kuna mtu (kiongozi) ambaye alikua na mtazamo, uchungu wa kweli wa wananchi wake, msikivu, anayependa kutumia vizuri hazina ya vichwa vya wataalam, sio mbinafsi, mkweli na mbunifu. Hivyo ni muhimu watanzania tujiweke kwenye maombi kila mtu na dini yake ili tupate kiongozi wa jinsi hiyo.
Mtu mwingine atasema maendeleo sio vitu tu bali na mambo mengine kama utu, haki za binadamu nk, hivi ulisikia wapi kwenye umaskini wa kutisha unaweza kupata haki? Utapateje haki ya tiba wakati watabibu na dawa hakuna, mwanafunzi atapateje haki wakati shule haina vitabu wala madawati, mkulima atapataje haki wakati hukuna pembejeo nk.
Kitu kikubwa kilichofanya tufike hapa ni kimoja tu yaani namna nzuri ya kuwapata viongozi wa kuchaguliwa na kuteuliwa ambao wangesaidia kulinda rasilimali na ustawi wa wananchi. Naungana na watu wengi wanaosema kwamba hakukuwa na umakini wa kubadilisha mfumo kutoka kwenye chama kimoja kwenda vyama vingi. Nashauri tusiweke nguvu nyingi sana na rasilimali nyingi ili kuharakisha katiba mpya ina andikwa kabla ya 2015. Tunaweza kuanza kwa awamu wakati mambo mengine yanaedndelea. Naungana na jukwaa la katiba kwamba haitaleta tija kama huu mchakato utaharakishwa.
Kipaumbele kwa sasa ni amani wakati tunaelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na baadaye uchaguzi mkuu. Na amani itakuwepo tu kama uchaguzi utakua huru na wa wazi (ionekane machoni pa wananchi kuwa ni huru na wazi). Kwa muda uliobaki tuanze kwanza na hili.
Naomba tume ya katiba iwasikilize wadau (km jukwaa la katiba wanavyoshauri) kwa mtazamo chanya. Mchakato uendelee kama kawaida bila kuharakisha. Ninavyomwelewa mzee wetu jaji warioba (mwenyekiti) ni miongoni mwa watanzania wenye ushawishi, uweledi, uadilifu na usikivu, hivyo atasikiliza maoni na kutafakari kwa kina kwa sababu mantiki iko wazi kwamba huwezi fanya mabadiliko makubwa kwa muda mfupi halafu utegemee mafanikio.
Mungu ibariki tanzania