Kwa nini tunaishi hivi !? Dunia na walimwengu waliona mini !?

Kwa nini tunaishi hivi !? Dunia na walimwengu waliona mini !?

Dig the EA

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2017
Posts
287
Reaction score
279
Salam Sana!
Nimekuwa nikijiuliza bila majibu sahihi kwa yanayotokea duniani na jinsi binadamu tunavyoishi!!
Kila binadamu anakua na kulazimika kutafuta pesa,bila pesa mtu haishi vizuri-swali ni kwamba hakuna maisha ambayo yangewekwa binadamu kuishi bila uwepo wa pesa na matumizi ya pesa!? Pesa imeonekana mataifa makubwa kutawala na kunyonya mataifa madogo! Huwawekea vikwazo vya kiuchumi(pesa) mataifa madogo ili kuzitawala!
Watu wenyewe ktk jamii tunathaminiwa kwa viwango vya kipato na pesa!

Pesa imekuwa chanzo cha matatizo duniani! Watu huuana sababu ya pesa! Taifa hushambulia na kupigana na lingine sababu ya pesa! Utu wa mtu huthaminiwa kwa pesa alizonazo! Pesa ni kama maisha na utu wa mtu!

Swali,je waliotengeneza mfumo wa matumizi ya pesa katika maisha ni akina nani !? Ni nini nia kuu na malengo ya mfumo wa kuishi kwa matumizi ya pesa duniani!? Je dunia na maisha yasingekuwepo bila matumizi ya pesa!? Je mfumo huu ulivyo ni halali kuwepo !?

Mwenye mawazo na maarifa ya kwa nini tunaishi hivi ,tafadhali-mawazo yako,tuelimishane!
 
Ukisoma kitabu cha Enoch kinasema Baada ya wale malaika 200 kushuka duniani waliwafundisha wanadamu kutengeza siraha,uganga,uchawi,unajimu, thamani ya madini yaliyopo ardhini,elimu ya nyota, FEDHA! etc Kitafute ukisome...
 
Pesa imerahisisha biashara.. zamani kulikuwa kuna biashara ya bidhaa kwa bidhaa lkn pesa imerahisisha hilo..
pia ktk kupata huduma pesa imesaidia pakubwa kiafya,kiusafiri n.k
pesa imekuwa si mbaguzi kwa mantiki hii.. kila huduma au bidhaa utaipata kwa fedha lkn ktk bidhaa kwa bidhaa inakuhitaji umtafute anaehitaji hiyo bidhaa ambapo na wewe unaihitaji bidhaa yake.. kama yupo mbali basi itabidi ubebe bidhaa yako umfate!,kama utahitaji usafiri na hakuna malipo ya hela itabidi ubebe na bidhaa ya kulipia huduma ya usafiri!.

Lengo nafikiri ilikuwa ni kupunguza mzigo..
mara nyingi kila jambo huwa na changamoto zake hivyo muda mwengine usilaumu pesa bali dhamira za wahusika!,kumbuka pesa tumeithaminisha tu ili kuturahisishia.. but the problem is us!
 
Sawa bro! Kwa nini biblia haijajikita kuzungumza kwa kina upatikanaji na matumizi mabaya ya hela na haikemei mifumo hii !!
 
Lkn hali ni mbaya I C ! Dunia haishikiki bila hela ! Nadhani kwa akili iliyopo kwa wanadamu duniani-wanaweza tengeneza mfumo mwingine wa kuishi!!
 
Mimi huwa najiulizaga kitu kimoja tu kuhusu pesa.Inakuwaje haya makaratasi na sarafu yanakuwa na thamani ya kuweza kukupatia chochote.Dunia ina siri nyingi sana tusizozifahamu.Tupo tupo tu!
 
Fedha ni njia ya kumiliki mali inayohamishika.unauza nyumba unapewa pesa yenye thamani ambayo wewe na unayemuuzia mumekubaliana kuwa ndiyp thamani ya hyo nyumba.
Kwahyo wa kulaimiwa kwa hayo matatizo uliyoyataja hapo juu ni wale waliosababisha kuwapo na mfumo mbaya wa uchumi.upatikanaji na utumiaji mbaya wa pesa/mali lawama ni kwa huyo mtumiaji.
Tunaweza mimi na wewe tukapewa kwa mfano milioni milioni.wewe ukaitumia kulipia mtoto ada mie ya kwangu nkaihongea na kuitumbua batani sasa hapo mwenye shida nani pesa ama mtumiaji?
 
Pesa imerahisisha biashara.. zamani kulikuwa kuna biashara ya bidhaa kwa bidhaa lkn pesa imerahisisha hilo..
pia ktk kupata huduma pesa imesaidia pakubwa kiafya,kiusafiri n.k
pesa imekuwa si mbaguzi kwa mantiki hii.. kila huduma au bidhaa utaipata kwa fedha lkn ktk bidhaa kwa bidhaa inakuhitaji umtafute anaehitaji hiyo bidhaa ambapo na wewe unaihitaji bidhaa yake.. kama yupo mbali basi itabidi ubebe bidhaa yako umfate!,kama utahitaji usafiri na hakuna malipo ya hela itabidi ubebe na bidhaa ya kulipia huduma ya usafiri!.

Lengo nafikiri ilikuwa ni kupunguza mzigo..
mara nyingi kila jambo huwa na changamoto zake hivyo muda mwengine usilaumu pesa bali dhamira za wahusika!,kumbuka pesa tumeithaminisha tu ili kuturahisishia.. but the problem is us!
[emoji122][emoji122][emoji122]
 
Sawa bro! Kwa nini biblia haijajikita kuzungumza kwa kina upatikanaji na matumizi mabaya ya hela na haikemei mifumo hii !!
Imekemea sana ktk upatikanaji usio sahihi na matumizi ya mabaya, kumbuka habari za watoza ushuru na matajiri waliojilimbikizia mali kwenye maghara huku wengine wakiteseka na kufa njaa, biashara ya ukahaba pia imezungumziwa sana.
 
Swali maridadi ! Yale ni makaratasi tu ,lkn yameaminishwa na kufanywa ya thamani kuliko kawaida! Kuna Siri hapo!!
 
Ila kama mfumo unaonekana tatizo na ukiwakandamiza wengi ungefaa kubadilishwa!
 
Hakuna sehemu Mungu(kama yy ndo anataka tubadilishane) alisema mpaka lazima tubadilishane Kwa pesa !!
 
Pesa na utawala vifutwe-narudia vifutwe,uone kama matatizo na dhambi havitapungua duniani!!
 
Hongera kwa kukaa na kujiuliza swali muhimu sana.

Hata ivo naweza nisifikie maarifa unayozungumzia ila nataka kusema Huu mfumo wa Pesa ,ulianzishwa na Mungu mwenyewe , ingawa wakat anauanzisha hakuitaja Pesa km means ya kuishi. , alipowaumba Adamu na Hawa,kwakua alijua wanakaa na kuishi bure aliwambia ivi ""Muilime busatan na muitunze"" nahii ikawa km pesa ,yaan ili ule nilazima uilime na uitunze bustani.

Hata ivo mambo yalibadilika muda mchache baadae walipofanya dhambi ,Mungu akawambia "utakula kwa jasho" na akawafukuza toka Adeni.

Sasa hapo ndo mambo yakabadilika ,nakuanzia hapo ikawabidi wahangaike ili waipate iyo pesa ili mwisho iwasaidie kula nakuyakimu matatizo yao
 
Ndo maana nikasema ingebidi kwenye maandishi ya biblia ingebidi ikemee sana pesa ! Lkn imegusa kdogo tu kama alivyosema mchangiaji mmoja!

Kama ni Mungu,mbona hakutoa mwongozo kama alivyokuwa anatoa kwa mengine!? Mbona hakuwatokea mitume na watu wake kuhusu pesa !?
 
Back
Top Bottom