Kwa nini tunalia msibani?

Inapotokea nimeenda kwenye msiba ambao haunihusu moja kwa moja huwa nalia hata kama marehemu hakuwa na faida kwangu.
Nahisi huruma pale ambapo ameacha watoto au watu wengi walikuwa wanamtegemea.
 
huwezi amini mie nilienda msibani badala ya kumlilia yule merehemu nikawa nakumbuka kifo cha rafiki yangu mpenzi na kubwaga chozi has ,lakini jibu ndo hilo kila mtu analia kwa sababu zake

ni kweli inatokea. Msiba mwingine unaanza kukumbuka watu wetu waliotutoka kitambo.
 
Sijawahi kulia kwasababu ya msiba. Ila huwa nina mawazo mengi juu mimi mwenyewe kuwa NITAKUFAJE?
 
Saa zingine akiishafariki mtu wako wa karibu unakuwa unaona hakuna zaidi ya hapo
 
Hili swali linaudhi sana sababu linakumbusha machungu yaliyopita. Ngoja ufiwe na mtu wa karibu utapata jibu
 
kulia inakuja tu automatic hasa ukishaona watu wanalia unajua mpaka wazungu wanalia ila sio kivile kama bongo!!!sema nshaona misiba mingine watu hawalii hasa akifa mzee mfano wa miaka kama 110 hv
 
Wanawake wanalia sana sababu hawana KOROMEO.ila wanaume hatulii sababu makoromeo yetu yanasound proof.
 
Mimi kusoma jumbe zenu hadi mwisho machozi yananilenga, wengine pia ni maumbile yao waliyoumbwa na Mungu, yaani machozi yanakuwa karibu sana, mfano mimi hata nikiona taarifa ya habari ya kusikitisha huwa nalia, yaani hadi mume wangu ananiambia usiangalie, hata mtu akinisimulia kitu cha kusikitisha machozi yananimwagika yaani na- feel kile kitu hadi natoa machozi, yaani kweli si-pretend inakuja automatically tu najaribu nisiwe hivyo lakini nashindwa. Nikiend kwenye msiba ndiyo kabisa mtu akilia kwa kuomboleza hata kama mtu simfahamu kabisa nitalia hadi macho yanakuwa mekundu, nikienda hospitali ndiyo usiseme nalia mwanzo mwisho nikiona wagonjwa yaani najawa na huzuni hadi watu wengine wanalia kwa kuniangalia tu
 
Mi binafsi kama nimeenda msibani na aliyekufa namfahamu na nilikuwa naye karibu then nitalia kwa kuona kuwa nitamkosa as company vinginevyo unajikuta unavuta hisia ya waliofariki waliokuwa karibu nawe na haswa kama ni ndugu, maana zile events zinafanana. Na ndiyo maana huwezi kwenda harusini then ukatimua kilio watu watakushangaa.!
 
wengine wanajiliza uwongo tuu kwa sababu ya hii kasumba ya ajabu kwamba usipolia msibani eti huna uchungu na huyo marehemu wakati sio kweli, mi naona inategemea tu na hulka ya mtu,wengine wanaumia lakin ni ngumu ku express feelings zao outside, wengine wanalia ukweli wengine wanapiga ukunga wa uwongo ili mradi tu na yee yumo!!
 

labda hayajawafika wenzetu....
 
<br />
<br />

Hayajakufika wewe subiri siku yako utalia tuuuuu......
 
Hakuna kinachotokea bila sababu. Nalia kwa sababu nitaukosa msaada wake, ninalia kwa sababu nitayakosa mapenzi yake, ninalia kwa sababu sitakuwa naongea naye.
Kuna wengine wanalia tu msiba, bila kujua ni nani kafariki. Hawa ni wale ambao katika maisha yao wamepatwa na masahibu na misiba iliyowagusa sana. Ni sawa kwa sasa na mkazi wa gongo la mboto, hata tairi la gari likipasuka atalia na kukimbia akidhani ni bomu kumbe siyo.
 
Kweli kwenye msiba kila mtu analia kwa reason yake, mfano mimi nikienda msiba yeyote namkumbuka marehemu baba yangu and i can not stop crying mpaka watu wanashangaa and they ask was he/she ur near one?!!!

Ishawahi kutokea dada mtu alipoteza kaka yake; huyo kaka alikuwa anamsaidia kifedha, those first tears were for the loss of the brother geninely but kilichofuata hapo dada mtu mwenyewe bila kujijua akaanza kusema nani atanisaida sasa etc etc na akaanza kulia...kusema ukweli watu walimshangaa sana.... this is ture tena huyo mtu ni mtu wa karibu na mimi nimeshuhudia hii kitu..........!!!
 


UNAPOELEKEA UTAULIZA KWANINI TUNAJISAIDIA HAJAKUBWA NYUMA BADALA YA MBELE!!!
Punguza kaspidi
 
kifo ni kitu cha huzuni sana na ukikifikiria lazima hisia za kuondoka kwa uhai zitaleta simanzi kubwa nafsini na kusababisha machozi au aina yoyote ya simanzi iwezekanayo kwa mwanadamu kukufika.
 
kuna mchungaji alifanya party kabla ya kuambiwa ni mwanae kaenda....huu ukoo iMEZIDI WA KIFALME UNAVYOJULIKANA KUFA WEWE UONE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…