Kwa Nini Tunawafundisha Watoto Wetu Mfumo wa Wakoloni Wakati Dunia Inaendesha Uchumi kwa AI na Code?

Prof_Adventure_guide

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2023
Posts
533
Reaction score
1,499
Wakuu, ukweli ni kwamba bado tumelala usingizi wa pono wakati dunia inapiga hatua kubwa kupitia Artificial Intelligence, Cloud Computing, na Automation. Mfumo wetu wa elimu wa sasa bado unazalisha wafanyakazi wa kuandika na kuhesabu (clerks) kama ilivyokuwa wakati wa wakoloni, badala ya kujenga critical thinkers na innovators wanaoweza kushindana kwenye soko la kimataifa la kidigitali.

Leo hii, skills ndio zinazomiliki dunia wala siyo vyeti vya makaratasi tulivyotundika ukutani. Vijana wetu wanapaswa kuelewa kuwa tech opportunities zipo nyingi mno, mtu anaweza akawa hapa hapa Dar es Salaam au Arusha, akawa anafanya remote work kwa kampuni za Marekani au Ulaya na kuingiza dollars ndefu kupitia ujuzi wa coding au digital marketing, mradi tu achague kuachana na mfumo huu wa kukariri mambo ya kizamani.

Hivyo basi, ni wakati sasa wa kujikomboa kifikra na kutumia mtandao kujisomea wenyewe self-taught badala ya kusubiri mitaala ya kizamani ibadilike. Tupunguze kupoteza muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii kwa mambo yasiyo na tija, badala yake tuweke nguvu kwenye kujifunza ujuzi wa sasa ili tusije tukawa watazamaji kwenye nchi yetu wenyewe wakati wengine wanatengeneza utajiri kwa kutumia akili na teknoloji
a.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…